SI KWELI Nyongo ya mamba ni sumu inayoweza kuua

SI KWELI Nyongo ya mamba ni sumu inayoweza kuua

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Naomba kuuliza wataalamu wa jamii check. Maisha yangu yote naamini kuwa nyongo ya mamba ni sumu, lakini kuna bosi wangu mmoja tumebishana vikali akidai kuwa si sumu bali ni nyongo tu kama ya binadamu. Ukweli ni upi?
crocodile.jpg
 
Tunachokijua
Kwa miaka kadhaa nyongo ya mamba imekuwa ikitajwa kuwa chanzo cha vifo vya watu, ambapo watu wengi wakiamini kuwa nyongo ya mamba ni sumukwa binadamu.

Januari 2015 nchini Msumbiji, watu 25 walitangazwa kufariki ambapo redio zilitangaza vifo hivyo kusababisha na nyongo ya mamba.

Hata hivyo, JamiiForums baada ya kupitia maandiko kadhaa ya wataalamu akiwemo Profesa Norman Nyazema ambaye ni mbobezi wa fani ya famasia, amekanusha imani maarufu hii baada ya kufanya utafiti wa kina wa jambo hilo.

Prof Nyazema, ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Limpopo nchini Afrika Kusini, amethibitisha kuwa nyongo ya mamba haina sumu kabisa, hata hivyo huwa inakausha na kuuzwa China kama dawa ya kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa

“Nyota ya mamba haina sumu hata kidogo. Kwa kweli, inakaushwa kwenye shamba la mamba huko Kariba na kusagwa kabla ya kuuzwa Uchina ambako inatumika kama dawa ya kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa,” Nyazema alisema.

Alisema alikuwa amefanya uchunguzi ambapo alitaka kugundua dalili zinazowakabili wale "waliotiwa sumu" na nyongo na ikiwa kunaweza kuwa na dawa ya sumu hiyo, alipogundua kuwa nyongo hiyo haina madhara.

Katika wasilisho la utafiti wake alisema iko miti ambayo ina sumu kali na hutumiwa na waganga wa kienyeji katika kuua watu katika matukio ya kunywa pombe kwa Pamoja ambayo ndio matukio yanayoripotiwa mara kwa mara.

Hata watu waliokufa nchini Msumbiji baada ya kunywa pombe yenye sumu, pombe waliyotumia ilithibitisha kuwa sumu iliyokuwa kwenye pombe ile haikuwa nyongo ya mamba.
Mimi nadhani ni sumu na kama sio sumu bas swali langu la moja kwamoja linakuja kwanini mamba akifa au aitegwa kwanini maliasili wanawahi kuchukua jyo nyongo na ngozi?
ngozi ya maba ni biashara ya serikali na wapo watu wanavibali vya kuwinda mamba sijui hivi sasa ..nyongo ushasikia inauzwa china kwa ajili ya nguvu za kiume kwa hio ni mali adimu..
 
Nami nimesikia Sana Simulizi kuhusu Nyongo ya Mamba, wanasema ukiweka kwenye Maji ni ColourLess(Haitoi Rangi) na wameenda mbali zaidi kwamba vilevile ni TasteLess(Haina Ladha). Wabobezi njooni huku Mtiririke kutujuza kuhusu Nadhalia hizi za NYONGO ya MAMBA!!
 
Nimeenda Zimbabwe nimekuta nyama ya mama inaliwa kwenye hoteli kubwa nikajiuliza wanadhibitije hiyo sumu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
ZImbabwe mbali, enzi zetu pale Bulyanhulu (KMCL) siku ya BBQ unawekewa lebo tu kwamba hapa ni vipapatio vya kuku, hapa ni seafood hapa ni mamba..!! Nikatest mamba nikaona poa tu..!!
 
ZImbabwe mbali, enzi zetu pale Bulyanhulu (KMCL) siku ya BBQ unawekewa lebo tu kwamba hapa ni vipapatio vya kuku, hapa ni seafood hapa ni mamba..!! Nikatest mamba nikaona poa tu..!!
Hiyo mamba inaladha gani
 
Naomba kuuliza wataalamu wa jamii check. Maisha yangu yote naamini kuwa nyongo ya mamba ni sumu, lakini kuna bosi wangu mmoja tumebishana vikali akidai kuwa si sumu bali ni nyongo tu kama ya binadamu. Ukweli ni upi?
crocodile.jpg
Du! uongo ukikuzwa na kuachwa bila kukanushwa hugeuka kuwa kweli, hili jambo toka nikiwa mdogo nilisikia ya kwamba, nyongo ya mamba ni sumu, kumbe ni dawa, yawezekana ni wajanja wachache walizusha ili waendelee kupiga hela kimya kimya.
 
ZImbabwe mbali, enzi zetu pale Bulyanhulu (KMCL) siku ya BBQ unawekewa lebo tu kwamba hapa ni vipapatio vya kuku, hapa ni seafood hapa ni mamba..!! Nikatest mamba nikaona poa tu..!!
Hebu tuongelee enzi za KMCL, na yule mzungu anaiitwa bongoman
Na ile timu ya mpira ilikuwa inatunzwa vizuri
Usinikumbushe Skanska na zile Scania zao, zinapigwa kidebe huku zinatembea
Nilipita hapo Tanzoro Drilling kama unaikumbuka
 
Swali ni hili; kama nyongo yake ni sumu na imo tumboni mwake ikitumika kusaga mafuta kwanini isingeanza kumuua yeye mwenyewe??--- kazi ya nyongo kwa wanyama wote ni kazi moja tu ya kusaga mafuta yanayoingia tumboni kana chakula hivyo kama nyongo ya mamba ingekuwa ni sumu basi hata Nyongo za Binadamu, Ng'ombe, kuku, Mbuzi nk nazo pia zingekuwa ni Sumu.
 
Duuh ila wanaosema ni sumu wanatumia ile hoja ya kwamba mamba ni kiumbe ambaye anakula kila kitu

Na hatafuni chakula chake bali anakimeza kizima kizima au mapande makubwa makubwa tu

Hivo kwenye umeng'enyaji wa chakula nyongo yake inakuwa na kazi nzito kuhangaika na takataka nyingi anazokula kiasi cha kuifanya itengeneze sumu
Tangu lini nyongo ikameng'enya chakula mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom