Naomba kuuliza wataalamu wa jamii check. Maisha yangu yote naamini kuwa nyongo ya mamba ni sumu, lakini kuna bosi wangu mmoja tumebishana vikali akidai kuwa si sumu bali ni nyongo tu kama ya binadamu. Ukweli ni upi?
- Tunachokijua
- Kwa miaka kadhaa nyongo ya mamba imekuwa ikitajwa kuwa chanzo cha vifo vya watu, ambapo watu wengi wakiamini kuwa nyongo ya mamba ni sumukwa binadamu.
Januari 2015 nchini Msumbiji, watu 25 walitangazwa kufariki ambapo redio zilitangaza vifo hivyo kusababisha na nyongo ya mamba.
Hata hivyo, JamiiForums baada ya kupitia maandiko kadhaa ya wataalamu akiwemo Profesa Norman Nyazema ambaye ni mbobezi wa fani ya famasia, amekanusha imani maarufu hii baada ya kufanya utafiti wa kina wa jambo hilo.
Prof Nyazema, ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Limpopo nchini Afrika Kusini, amethibitisha kuwa nyongo ya mamba haina sumu kabisa, hata hivyo huwa inakausha na kuuzwa China kama dawa ya kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa
“Nyota ya mamba haina sumu hata kidogo. Kwa kweli, inakaushwa kwenye shamba la mamba huko Kariba na kusagwa kabla ya kuuzwa Uchina ambako inatumika kama dawa ya kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa,” Nyazema alisema.
Alisema alikuwa amefanya uchunguzi ambapo alitaka kugundua dalili zinazowakabili wale "waliotiwa sumu" na nyongo na ikiwa kunaweza kuwa na dawa ya sumu hiyo, alipogundua kuwa nyongo hiyo haina madhara.
Katika wasilisho la utafiti wake alisema iko miti ambayo ina sumu kali na hutumiwa na waganga wa kienyeji katika kuua watu katika matukio ya kunywa pombe kwa Pamoja ambayo ndio matukio yanayoripotiwa mara kwa mara.
Hata watu waliokufa nchini Msumbiji baada ya kunywa pombe yenye sumu, pombe waliyotumia ilithibitisha kuwa sumu iliyokuwa kwenye pombe ile haikuwa nyongo ya mamba.