Nyongo ya Wallace Karia Rais wa (TFF) Kuhusu Mabadiliko Ya Kanuni za TFF

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
"Anayesema kanuni hazipo kihalali (Manara) kanuni hizohizo ndizo zinasema mwenye pointi nyingi awe bingwa, sasa kama mtu anasema hazipo kihalali ina maana ligi yetu ya msimu uliopita ilikuwa batili !"

"Mwaka huu usajili uliofanyika ni mkubwa sana, vilabu vyote vimekuwa na michakato mikubwa ya usajili, na wamesajili Wachezaji ambao watawasaidia"

"Ligi yetu ni miongoni mwa ligi nne ambazo zina hamasa kubwa Afrika, na sisi Tanzania tunavivutio vikubwa Duniani ambavyo wengine hawana na tuna Simba na Yanga ambazo wengine hawana"

"Mimi nategemea ligi yetu itakuwa ni bora sana kwa sababu ya usajili uliofanyika"

"Mashabiki na wadau tunaomba waheshimu kanuni. Sawa tunajua mitandao ipo kila mtu anaweza kutoa maoni ila ni vyema wakaheshimu taasisi kwamba tunayofanya tunatumia taaluma hatukurupuki"

"Kuna kanuni ambazo zinahusu nidhamu na maadili, hizi tumezikopi kutoka (FIFA) tukaziongeza kidogo kutokana na mazingira na zinatumika kila mwaka,, Kwa mfano kanuni za maadili na nidhamu hizi zimetengenezwa zaidi ya miaka (9) iliyopita"

"Sisi tuna nafasi ya kuboresha kanuni hizi kutokana na matukio yanayotokea au mabadiliko yanayotokea"

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Huyu Karia aliwapa GSM mkataba wa bei rahisi sana kuidhamini ligi, yaani bilioni mbili kwa miaka miwili. Aliwapendelea sana
 
"Anayesema kanuni hazipo kihalali (Manara) kanuni hizohizo ndizo zinasema mwenye pointi nyingi awe bingwa, sasa kama mtu anasema hazipo kihalali ina maana ligi yetu ya msimu uliopita ilikuwa batili !"

"Mwaka huu usajili uliofanyika ni mkubwa sana, vilabu vyote vimekuwa na michakato mikubwa ya usajili, na wamesajili Wachezaji ambao watawasaidia"

"Ligi yetu ni miongoni mwa ligi nne ambazo zina hamasa kubwa Afrika, na sisi Tanzania tunavivutio vikubwa Duniani ambavyo wengine hawana na tuna Simba na Yanga ambazo wengine hawana"

"Mimi nategemea ligi yetu itakuwa ni bora sana kwa sababu ya usajili uliofanyika"

"Mashabiki na wadau tunaomba waheshimu kanuni. Sawa tunajua mitandao ipo kila mtu anaweza kutoa maoni ila ni vyema wakaheshimu taasisi kwamba tunayofanya tunatumia taaluma hatukurupuki"

"Kuna kanuni ambazo zinahusu nidhamu na maadili, hizi tumezikopi kutoka (FIFA) tukaziongeza kidogo kutokana na mazingira na zinatumika kila mwaka,, Kwa mfano kanuni za maadili na nidhamu hizi zimetengenezwa zaidi ya miaka (9) iliyopita"

"Sisi tuna nafasi ya kuboresha kanuni hizi kutokana na matukio yanayotokea au mabadiliko yanayotokea"

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kwa maneno haya ni wazi Karia ameumia Yanga kuwa bingwa msimu uliopita. Nikiwaambia huyu ni Zuzu muwe mnaelewa. Kiongozi asiyejua kuchagua maneno ya kuongea kama si Zuzu tumuiteje?
 
Inabidi tumrudishe Malinzi wetu siyo?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Hata huyo Malinzi naye alikuwa chenga tu. Hana tofauti na Wallace Karia. Leodgar Chilla Tenga ndiye rais aliyejitahidi kadiri ya uwezo wake kuongoza TFF kwa haki, na kwa kufuata taratibu zilizo wekwa katika mpira wa miguu.

Enzi za utawala wake, manung'uniko kutoka kwa wadau, yalikuwa ni machache sana ukilinganisha na uongozi wa Jamal Malinzi na huyu Wallace Karia.
 
Back
Top Bottom