Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,669
- 8,268
"Anayesema kanuni hazipo kihalali (Manara) kanuni hizohizo ndizo zinasema mwenye pointi nyingi awe bingwa, sasa kama mtu anasema hazipo kihalali ina maana ligi yetu ya msimu uliopita ilikuwa batili !"
"Mwaka huu usajili uliofanyika ni mkubwa sana, vilabu vyote vimekuwa na michakato mikubwa ya usajili, na wamesajili Wachezaji ambao watawasaidia"
"Ligi yetu ni miongoni mwa ligi nne ambazo zina hamasa kubwa Afrika, na sisi Tanzania tunavivutio vikubwa Duniani ambavyo wengine hawana na tuna Simba na Yanga ambazo wengine hawana"
"Mimi nategemea ligi yetu itakuwa ni bora sana kwa sababu ya usajili uliofanyika"
"Mashabiki na wadau tunaomba waheshimu kanuni. Sawa tunajua mitandao ipo kila mtu anaweza kutoa maoni ila ni vyema wakaheshimu taasisi kwamba tunayofanya tunatumia taaluma hatukurupuki"
"Kuna kanuni ambazo zinahusu nidhamu na maadili, hizi tumezikopi kutoka (FIFA) tukaziongeza kidogo kutokana na mazingira na zinatumika kila mwaka,, Kwa mfano kanuni za maadili na nidhamu hizi zimetengenezwa zaidi ya miaka (9) iliyopita"
"Sisi tuna nafasi ya kuboresha kanuni hizi kutokana na matukio yanayotokea au mabadiliko yanayotokea"
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app