Nyota ya Mandonga imeanza kufifia, sasa ni zamu ya Zumaridi na DJ Ally B

Bondia wetu Mandonga taratibu anaanza kutoka nje ya reli. Ule umaarufu wake umeanza kupotea kiaina. Yeye sio wa mwanzo wala sio wa mwisho katika watu walioibuka na ku-vibe kisha kupotea.

Huko nyuma alishawahi kuwepo babu wa loliondo, nabii tito, pierre likwidi, Dr. Shika na wengineo wengi.

Sasa naona zamu ya Zumaridi ambaye anapewa airtime na media ya Tanzania kuongea vitu vya kufikirika.

Pia kuna mtu anajiita DJ Ally B almaarufu Profesa au Asumani.
Yeye hupiga kelele na miluzi akiwa kwenye gari lake...basi nae kawa maarufu.

Wakati ni ukuta!
Mungu wa Mbinguni hujua nyakati na vitu vya kuliwaza waja wake wa Tanzania.Hapendi Watanzania wakose furaha hata kidogo.
 
Mandonga in downtown Kampala.
Screenshot_20230325-022951.jpg
 
Si ndio, kina Mb doggy na Z anto huko youtube wana fans kibao kutoka kenya, wkati huku tupo busy na kina Mondi kila siku
Wote hao akina Diamond, Ali Kiba wamekuzwa na Kenya.

Kumbe Z-Anto na Mb Doggy bado huko 254 wanapiga show hatari? Huku 255 hata wakipiga Bar au Banda umiza kwa Kiingilio cha 2,000 Tsh(110 Ksh) wanaweza wasipate watu ila kwa Kenya wanaweza waka sold out show.
 
Kwetu tunafuatilia uzuri wa muziki sio kulea majungu na wasanii na ndio maana akina Rose Muhando wanaimba kutushukuru, kwenu huko mnawashusha kwa majungu, huwa nafuatilia comments zenu kwa Diamond aise huwa mnamtukana sana huyo dogo wa Tandale, sijawahi kuelewa au kujua nini kosa lake licha ya yeye kubuni ajira nyingi tu kwa Watanzania.

Hapana majungu Mkuu ,na sisi tunapenda mziki mzuri ,"dayamondi" na Rose washashuka kimziki ndiyo maana "dimondi" amejikita sana kwenye biashara nyingine muziki anafanya kwa ajili ya kuwafurahisha "mambulura wake" wasimsahau ,Rose lazima aishukuru 254 maana mmemtibia mpaka amepona! Dogo wa Tandale anatukanwa kwasababu na yeye ana timu yake ya kutukana watu wanaosupport wasanii wengine.

Wasanii wa huku 255 wakishaanza kushuka kimziki wanakimbilia huko kwenu 254....Z-anto/Mb Doggy walishasahaulika kama ni wasanii , Mandonga mtu kazi huku ashaanza kupotea ndiyo maana anaanza kutafuta chocho huko 254 na 256.
 
Watanzania tumezidi kuwa wachawi
Unalala unamka unawaza nyota ya mwanaume mwenzio inashuka

Wivu au roho mbaya tu
Ilishuka ikipanda we umemsadia nini? Au inakusaidia nini?

Maisha saiv hela ngum tukomae kuisakama hela
 
Hapana majungu Mkuu ,na sisi tunapenda mziki mzuri ,"dayamondi" na Rose washashuka kimziki ndiyo maana "dimondi" amejikita sana kwenye biashara nyingine muziki anafanya kwa ajili ya kuwafurahisha "mambulura wake" wasimsahau ,Rose lazima aishukuru 254 maana mmemtibia mpaka amepona! Dogo wa Tandale anatukanwa kwasababu na yeye ana timu yake ya kutukana watu wanaosupport wasanii wengine.

Wasanii wa huku 255 wakishaanza kushuka kimziki wanakimbilia huko kwenu 254....Z-anto/Mb Doggy walishasahaulika kama ni wasanii , Mandonga mtu kazi huku ashaanza kupotea ndiyo maana anaanza kutafuta chocho huko 254 na 256.

Mondi ameshukaje kimziki, siku chache tu juzi hapa kaachia kibao cha Zuwena na naona kimepata mamilioni ya views duniani.
Muziki wowote hata wa zamani, ikitokea umefanywa kwa ustadi basi utasklizwa miaka yote, huyo Z-Anto mpaka leo napenda sana ngoma yake.
Kimsingi wewe enjoy ngoma, achana na msanii.....
 
Mandoga ndo anaondoka kwenye mfumo mdogo mdogo soon atasahaulika kama piere liquid
 
Back
Top Bottom