Nyota ya Msuva ni "nyota ya kanda ya mashariki"...

Nyota ya Msuva ni "nyota ya kanda ya mashariki"...

Nanoli

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
3,735
Reaction score
5,974
Mshambuliaji wa Timu ya Difaa al Jadida ya Morocco ambaye ni raia wa Tanzania, Saimoni Msuva ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ya mwezi wa Agosti ndani ya klabu hiyo.

Msuva aliyejiunga na timu hiyo mapema mwezi Agosti baada ya kuuzwa na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC , aliingia katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo sambamba na mchezaji mwenzake kiungo mkabaji Said Mohamedi.

Baada ya kura zilizopigwa na wanachama wa klabu hiyo, Msuva ameibuka kidedea kwa kura 268 na kumuacha mwenzake akipata kura 129.
 
Weka Na Suporting Picture Basi Hata Akipewa Hiyo Tuzo Ama Kaishika Tu Ili Kuupa Uzito Kidogo Uzi Wako....
 
ana maana gani kuwa ni "nyota ya kanda ya mashariki"? msuva asili yake ni kanda ya mashariki?
 
Kwa kuongea tu tupo vzr sana ndio kwanza hata miez miwili hana iweje achukue tuzo ya mchezaj bora wa mwez agost?
 
Back
Top Bottom