Nyufa , weaknesses walizonazo Chadema ambazo CCM na serikali mara kwa Mara huzitumia kuwavuruga

🚮🚮🚮
 
CCM ilishakufa au ilishajichokea.

Kwasasa CCM haifanyi kabisa siasa.

Siasa zote za CCM kupambana CHADEMA zinafanywa na taasisi za umma na Dola, kuanzia:
  • Polisi
  • Mahakama
  • Uhamiaji
  • Wakurugenzi
  • RCs/DCs
  • Goons/Mahuni
  • Msajili wa vyama

Ukiangalia hao wote wako ULINGONI wanapambana na CHADEMA.

Na hapa issue siyo CHADEMA bali ni UMMA unaotafuta MBADALA. Jata leo CVM ikimchukua Heche, Lema, Lissu, Mbowe wahamie CCM, unafikiri upinzani utakufa??

Maana CHAGUZI ni kwaajili ya watu na siyo WANASIASA.


Ukiangalia kesi zote za Mahakamani, huwa yanatumika MABAVU tu, wala siyo kwamba kuna taratibu za kisheria hufanyika.

Mwisho, CCM wanapambana na kitu amabacho HAWAKIJUI.

CHADEMA ni Jina tu.

Ilikuwepo NCCR MAGEUZI, ikaja CUF na sasa CHADEMA.

Issue siyo vyama ni WATU.

Siku zote watu wanaokupinga watakuwepo tu. Heche na Lissu wasipokuwepo, Upiznani utakuwepo tu, hata kama ikibaki CCM pekee dunia hii MILELE na MILELE, upinzani utakuwepo.

Wameuawa kina Ally Kibao, Mawazo, Mdude, Ben Sanane, Kimepungua nini???

Utaua kila mtu???
 

Mitandaoni upepo upo kivingine.
Watu kujitambulisha kama CCM kwa SASA wengi wanaona ni kipengele
 
Ungejipa nafasi ya kuangalia cdm ya Mbowe na Lisu kwanza. Cdm ulliyoizungumzia kwa asilimia kubwa ni ya akina Mbowe na Mrema.

Hiyo ya Mbowe ndio inaipasua Chadema.
Chadema wakifanikiwa hapa basi huko mbele kweupe
 
weakness kubwa za Chadema ni 1 moja hawana pesa zao kujitosheleza wanategemea serikali kuishi 2 hawana upendeleo wa dola na changamoto kubwa mifumo haiwapi uwanja sawa. Nguvu yako kubwa ni kukubalika na wananchi na jumuiya ya kimataifa.

Sahihi
 
nimelisema sana hili humu na watu wamekuwa wakinitukana. changamoto kubwa ya chadema ni hizi;

1. wanatumia nguvu badala ya akili, wakiumia wanaomba huruma kwa wananchi na nchi za nje badala ya kupambana wenyewe. wanaowategemea wakiwapa kisogo wanakwisha.

2. mamluki, wengi waliomo ndani wamenunuliwa, vikao vyote viko uchi na mipango yao yote ipo uchi.

3. pesa, chama hakina pesa.
 
Hata mimi nikienda leo CHADEMA utashangaa yananipa Uwenyekiti wa chama Taifa pamoja na kunipa nafasi ya kugombea Ubunge.
Kwani hiyo ni ajabu?
Huwajui wana Chadema ambao walienda huko ccm wakapewa nafasi, mbona ni wengi mno eg Kitila Mkumbo, Waitara, Mollel, nk?
 

Sahihi kabisa.
Ukishaingia vitani kubali yote. Pambana mpaka dakika ya mwisho
 
Ambacho wamekifanya kina Mrema na kigaila kwa kweli ni huzuni.

..kuna kukata tamaa pia.

..watu wamefanya harakati for 20++ years.

..Kuna wakati wanaweza kupata mashaka kama watafanikiwa au la.

..Mrema, Kigaila, Mdee, Msigwa, wote walijitoa kwa kadri walivyoweza na inawezekana walifika mahali wakakata tamaa.
 
Wanafanyaje kutoka hapa?
Hili linahitaji tafakuri kubwa, sio lelemama. Mizizi ya ccm imezama ndani sana, kuing'oa huenda hata damu ikamwagika. Ni miaka zaidi ya 40 ccm wapo tu, tunatumia katiba ya miaka 40+ iiyopita ambayo inampa mtawala umungu mtu.

Hata hivyo bado nawapongeza wenye uthubutu huko upinzani, sio rahisi.
 
Naona wamekulipa kukutuma ufanye spinning mwanawane.

Waambie mabwana zako CCM No Reforms No Elections.

Upuuzi wanaofanya wanaweza kuufanya tu kwa sababu wamehodhi mfumo wa hovyo ambao utaondoka tu through Reforms
 

Tayari damu za wanachadema zimemwagika kwa watu kadhaa.
Mbinu za kawaida zimeshindikana.
 
Punguza uchawa dogo 🤔🤔 acha kujitoa ufahamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…