A
Anonymous
Guest
Hufika Kawe wakiwa na matumaini ya kupata huduma za kiroho, na kwa wengi wao matumaini hayo hutimia. Lakini kwa baadhi, safari hiyo hubadilika na kuwa mapambano ya kutafuta malazi, chakula na nauli ya kurejea nyumbani. Ni katika mazingira hayo ndipo huibuka simulizi ambazo hazisikiki jukwaani, za watu wanaodai kulazimika kufanya maamuzi magumu ili kujikimu na kupata mahitaji muhimu.
Lakini yapo mambo ambayo huwezi kuyaamini kwa kusimuliwa mpaka uyashuhudie mwenyewe.
Andiko hili halijajengwa juu ya simulizi za kusadikika, bali linategemea mahojiano na ushuhuda wa watu wanaodai kushuhudia yanayotokea wakati wa mikusanyiko mikubwa ya ibada na semina zinazofanyika katika viunga vya Tanganyika Packers, Kawe.
Jordan (si jina lake halisi) ni kijana mwenye umri wa miaka 27 anayejishughulisha na usafirishaji kwa pikipiki, maarufu kama bodaboda. Kituo chake cha kazi kipo Kawe, jirani na eneo ambalo mikusanyiko hiyo hufanyika.
Kwa mtazamo wake, kila kunapotangazwa mkusanyiko mkubwa wa kidini, shughuli za kiuchumi huongezeka. Nyumba nyingi katika maeneo ya Kawe hasa makazi ya vijana wasio na familia, anasema, hubadilishwa kuwa malazi ya muda kwa wageni wanaofika kutoka mikoa mbalimbali.
Hata hivyo, nyuma ya ongezeko hilo la shughuli za biashara, Jordan anadai kuna simulizi nyingine ambayo si wengi huizungumza.
Anasema baadhi ya waamini hufika mapema ili kuhakikisha hawakosi nafasi kwenye mkusanyiko, lakini wengi wao hukumbwa na changamoto ya kukosa sehemu ya kulala au fedha za kugharamia malazi na chakula. Ndipo, kwa mujibu wa maelezo yake, baadhi ya vijana huliona hilo kama fursa.
"Kuna wanawake wengi nimeshawahi kuwapa hifadhi nyumbani kwangu. Kipindi cha makongamano makubwa unaweza kukaa naye hadi siku tatu. Wengi wanakuwa hawana uwezo wa kulipia lodge, hivyo anapopata mtu wa kumsaidia, wakati mwingine anakubali hata mazingira ambayo asingeyakubali katika hali ya kawaida," anadai Jordan.
Madai yake yanafanana na yale ya kijana mwingine anayefahamika kwa jina la utani la Baba J.
Kwa mujibu wa Baba J, amewahi kukutana na waamini waliobaki Kawe baada ya makongamano kumalizika kwa sababu walikosa nauli ya kurejea nyumbani.
Anadai kuwa si wote waliopoteza fedha zao; wengine walifika wakiwa na nauli ya kwenda pekee, wakiamini kwamba watapata namna ya kurejea baada ya ibada kumalizika.
"Mara nyingi makongamano yanapoisha, kuna watu hubaki wakizunguka kwa kukosa nauli ya kurudi makwao. Wapo wanaosema fedha zao zimepotea kwenye mkusanyiko, na wengine hukiri walisafiri bila kupanga nauli ya kurudi."
Anasema hali hiyo huwafanya baadhi yao kuwa katika mazingira magumu.
"Wakikutana na watu wenye nia mbaya, ujikuta kwenye mazingira ya kutumiwa kwa sababu wanahitaji fedha za kula au za kurejea nyumbani. Ukizungumza na baadhi ya waendesha bodaboda au wafanyabiashara wa maeneo ya Kawe, utasikia simulizi zinazofanana na hizi," anadai.
Uchunguzi uliofanywa na Mzalendo umebaini kuwa baadhi ya waamini hufika Kawe siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza kwa mikusanyiko hiyo. Wengi wao wanasema hufanya hivyo ili kuepuka changamoto za usafiri zinazoweza kuwafanya wakose ibada au semina.
Lakini kadiri siku zinavyoongezeka kabla na baada ya mkusanyiko, ndivyo gharama za chakula, malazi na usafiri zinavyozidi kuwa mzigo kwa baadhi yao.
Katika mazingira hayo, si jambo la ajabu kuona baadhi ya waamini wakilala maeneo ya wazi, huku wengine wakisaka msaada wa mahali pa kulala kutoka kwa watu wasiowafahamu. Wakati mwingine wanawake huonekana wakikesha nje wakiwa na watoto wachanga, jambo linaloibua maswali kuhusu usalama na ustawi wao.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo pia wanasema wamewahi kuombwa hifadhi na wageni waliofika kwa ajili ya mikusanyiko hiyo.
Aidha, baadhi ya watu waliokaribu na eneo la kanisa wanadai kuwa waumini wanaotaka kulala ndani ya eneo la kanisa huzuiwa na walinzi kwa maelekezo waliyopewa. Mzalendo haikuweza kuthibitisha sababu rasmi za utaratibu huo.
Baadhi ya wakazi wa Kawe soko jipya wanasema kuwa baadhi ya waamini hupiga kambi katika eneo hilo wakiwa na watoto, huku wakikosa mahitaji muhimu kama chakula.
Mama lishe mmoja (jina tunalihifadhi) anayejishughulisha na uuzaji wa vitafunwa, ikiwemo mihogo, anasema:
"Wapo watu wengi hapa wanaohangaika kupata chakula. Baadhi yao hulazimika kuja kwetu kujitolea kufanya kazi ili wapate chakula chochote, maana wengine unawakuta wamekuja na watoto."anasimulia.
Anaongeza kuwa si jambo la ajabu kuwaona baadhi yao wakiokota chupa za plastiki kwa ajili ya kuuza ili wapate fedha za kujikimu na kuendelea kubaki eneo hilo wakisubiri shughuli za ibada.
"Mama na Watoto wadogo wanalala nje"
Uchunguzi umebaini uwepo wa baadhi ya akinamama wakiwa wanaishi chini ya miti pamoja na watoto wao wadogo, wakilazimika kupata huduma zote ikiwemo chakula wakiwa katika mazingira hayo.
Mmoja wa wanawake waliokutwa eneo hilo anadai kuwa amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo kwa muda mrefu. Anasema alipata nauli ya kuja, lakini hakuwa na fedha za kurejea nyumbani, akitarajia kutumiwa nauli baada ya kufika.
"Natokea Singida. Mimi kule nafanya kazi ya kilimo. Nimekuja hapa na sasa nina siku tatu nalala chini ya mti nikiwa na mtoto wangu. Nangojea nitumiwe nauli ili niondoke, maana kilichonileta tayari kimekamilika," anasimulia mama huyo mwenye watoto wawili.
Anadai kuwa ameamua kuendelea kuishi eneo hilo kwa sababu hana uwezo wa kugharamia malazi. Anasema pia yupo pamoja na wenzake.
"Kuna wengine wameenda kuomba hifadhi kwa watu wa maeneo ya karibu, lakini wanadai wamekutana na vitendo visivyofaa. Mimi naona ni bora nilale chini ya mti kuliko kwenda kuishi kwa mtu nisiyemfahamu nikiwa na mtoto."
Hali hiyo inaweza kuibua mjadala mpana kuhusu wajibu wa waandaaji wa mikusanyiko mikubwa inayohusisha maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Je, pamoja na maandalizi ya kiroho, kunapaswa pia kuwepo mfumo wa kushughulikia changamoto za dharura kama malazi salama, msaada kwa wanaopoteza nauli, huduma kwa wanawake wenye watoto na utaratibu wa kuwasaidia waamini wanaokwama baada ya mikusanyiko?
Maswali hayo yanaendelea kutafuta majibu
Kwa sababu wakati maelfu ya waamini huondoka wakiwa na matumaini mapya ya kiroho, simulizi za baadhi ya waliokwama njiani zinaonyesha kuwa safari ya imani, kwa wengine, huambatana pia na gharama ambazo hazionekani kirahisi.