DOKEZO Nyuma ya pazia: Wanayopitia Waamini wanaofika kwa Mwamposa kwenye makongamano ya kidini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hakuna mtu aliyesema nini kifanyike. Mwamposa hawezi wamudu kuwalisha,malazi,nauli kwa watu wote wale, na akifanya hivyo navyowajua wa Tz watajazana mamilioni hapo.

Hawezi wakataza pia kwenda(unamfukuzaje mteja?), na serikali haiwezi ingilia kati sababu ni mtu wao wa karibu.

Lakini kwanini uende kwa design hiyo haujui unaenda kuishije hizo siku zote? Ratiba uiandae wewe, harafu huruma uitegemee kwa nani?
 
Tapeli huyo, kama anaweza kuwaombea (kwa anavyodai) wagonjwa wakapona basi suala la kuwalisha ni dogo sana.

Kuhusu makazi ilipaswa walale bure hapo ktk hilo jengo lake haramu la ibada za kishetani mnaloita kanisa sijui TAKATAKA gani, kama wanavyofanya baadhi ya makanisa au dini ya uislamu mtu yeyote anaruhusiwa kulala msikitini akikosa mahala pa kulala, sasa huyo tapeli anashindwa nini?, au anaogopa kushitukiwa kuonwa anayoyafanya ktk hilo jengo?, au hana huruma kwa wateja wake?.

Hakuna na ayupo aliyewai kuombewa na kupona kutoka kwa maombi ya huyo jamaa, watu waache kudanganywa, wasome maandiko ya dini zao.

Shida yote hii ni Serikali kukosa uhalali wa kuongoza taifa, ndipo huibuka mambo ya hovyo kama haya, sheria na taratibu zilitakiwa kudhibiti hii mikusanyiko ya kidini, pia elimu sahihi na huduma bora kama zingetolewa tusingekuwa na huu upuuzi na ujinga wa watu kutegemea miujiza badala ya matibabu/huduma sahihi za kiafya na kiuchumi
 
Unajua changamoto wanazozipata mahujaji huko mji mtakatifu makkah zipo kivumbi achilia mbali vifo vyakikanyagana sion tatizo watu wakipitia hayo katika kupambania wanachokiamini kwenye wengi pana mengi, watu washawahi kulala wati sita chumba kimoja lodge dodoma kwenye interview ya TRA na wengine walilq bar plus kutembea kwa miguu umbali mrefu maana boda zilikua hazishikiki kutokana na population ya ghafla iliozid miundombinu sasa huyu mwandishi wa mzalendo ndio kaona kapiga bonge la investigative journalism bomboclaat
 
Kwa nini mtume wao asiwarudishie kidogo ktk sadaka alizokusanya kama msaada kwao kwa kuwanunulia vyakula na malazi ili kutimiza yale aliyoyafanya Yesu kuwapa makutano shibe na usiku salama kwenye mikusanyiko?
Kama walimchangia nauli ya kutoka mbeya Kuja dar na yeye atawachangia.
 
Nilikuwa nafikiria kama ww .

Waumini wa mikoani ni muhimu wapewe information zaidi kuhusu Mazingira watakayoyakuta. Ili wajiandae.
Hii itapunguza hizi ghasia.

Ni kweli wanateseka.
 
Ikiwa unataka kujibu au kuchochea mjadala kwa njia ya kit
Binafsi naomba kuchangia kidogo kuhusu hili.

Mikutano mikubwa ya kidini inaleta watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiwa na matarajio ya kupata msaada wa kiroho. Hata hivyo, inapofanyika mikusanyiko ya maelfu ya watu, ni muhimu pia kuzingatia usalama na ustawi wao baada ya ibada.

Waandaaji wanapaswa kuwa na utaratibu wa kushughulikia changamoto za dharura kama malazi salama, msaada wa usafiri kwa waliokwama, huduma kwa wanawake na watoto, pamoja na mifumo ya kuripoti na kushughulikia vitendo vya unyanyasaji endapo vitatokea.

Hii sio kupunguza thamani ya huduma za kiroho, bali ni kuhakikisha kuwa utu, usalama na heshima ya kila mshiriki vinapewa kipaumbele.

Ikiwa madai haya ni ya kweli, yanaibua swali muhimu kuhusu wajibu wa waandaaji wa mikusanyiko mikubwa.

Mafanikio ya mkutano hayapaswi kupimwa kwa idadi ya washiriki pekee, bali pia kwa namna washiriki wanavyolindwa kabla, wakati na baada ya mkutano.

Madai yanapaswa kuchunguzwa kwa haki, na hatua stahiki zichukuliwe pale panapobainika mapungufu, huku ikizingatiwa kuwa ushuhuda wa baadhi ya watu haupaswi kuchukuliwa kama uthibitisho wa moja kwa moja wa hali ya jumla bila ushahidi wa kutosha.
 
Hao wanaotafuta ajira sio haya mambo ya imani, na hilo la ajira sio endelevu kama hili.
 
Mada ya mtoa mada nikweli
Elim
Ilm
Elim.

Ofisi za ustawi na police zifunguliwe hapo chap.

Ni dsm nizam usiku ni majanga nikipata mda nitaeleza kisa cha katoto kakike. Uhasibu kutudanganya umri 19 na kuondoka na boda
Elim.ilm
 
Mwamposa tapeli sana. Kwenye biblia ambayo huyu mwamposa anaitumia(kama ni kweli), Yesu alipoona makutano(watu) wamekaa nae muda mrefu na wana njaa alifanya muujiza wa chakula na watu wanaume 5000(pasipo kuhesabu wanawake na watoto) walikula na kusaza.

Mwamposa anakaa nao usiku kucha, anawalipisha fedha za maji ya "upako" na sadaka za kujimaliza halafu anawaacha wanazagaa kukipambazuka.

"Serikali" hadaa nayo ipo inasubiri mpaka maafa yatokee ili waje na kauli ya "tunafanya uchuguzi"

Haya mambo ndio maana kagame kapiga stop. Kaona ni kuwatapeli tu wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…