KERO Nyumba 2,450 zilibomolewa Mitamba-Kibaha, CAG kaibua upigaji wa Halmashauri eneo hilohilo, je, hatukutendewa haki?

KERO Nyumba 2,450 zilibomolewa Mitamba-Kibaha, CAG kaibua upigaji wa Halmashauri eneo hilohilo, je, hatukutendewa haki?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mwananchi kutokea Pwani, Wilaya Kibaha kero yangu ni kuwa ninachukizwa na ukiukwaji na ukatili tuliofanyiwa na Serikali kuvunja nyumba takribani 2,450 wakidai ni wavamizi waliovamia pori maeneo Mitamba Kata ya Pangani kisha wakapima maeneo na kuuzia watu wengine.

Juzi tunasikia Ripori ya CAG ikieleza kuwa kuna pesa hazikuingia kwa Serikali bali kwa watu binafsi, hili suala Wananchi tumelishughulikia kutafuta utatuzi kila tunapo kanyaga wanasema hawana taarifa kama watu walibomolewa.

Inamaana uongozi haujui ni viwanja gani na mandhari ya viwanja hivyo, ilikuwaje sisi wananchi tumekwisha elewa kuwa serikali ipo kwaajili kukandamiza wananchi wake.
 
Back
Top Bottom