Mkuu J.Kuu, watu wanacho sahau ni kwamba kinacho fanyika ni kwamba unangalia nyumba ulijengwa kwa gharama gani, je tangu wakazi/tenants waanze kulipa kodi, je, sum total ya kodi over the years ilishavuka return of investment na kuhanza kuvuna faida au la?
Tukiweka maanani kwamba nyumba hizo zilijengwa zamani sana ni dhahili ziliisha jilipa na faida juu, hivyo Serikali ikiwahuzia wapangaji kwa bei ya kawaida haitapata hasara after all lengo la Serikali lilikuwa ni kuwawezesha wapangaji kumudu kununua nyumba hizo kwa bei ndogo siyo Serikali kupata faida ya ziada.
Zamani hata National Housing Corp iliwahi kuwauzia tenants nyumba, hata Ulaya specifically Uingereza huwauzia wapangaji Council flats bila ya kujali kama mpangaji ni raia au la - what counts ni hela yako tu.
Kwa hiyo suala hili ya nyumba za Serikali tusilivalie njuga sana, hakuna haja ya kulichukulia kama ni suala la uhaini vile, mimi mpaka sasa nina imani kwamba Serikali ilikuwa na nia safi kuwauzia wapangaji nyumba.
..nimeuliza swali ambalo hujalijibu.
..je, mkapa, kikwete, sumaye, lowassa, magufuli, au mtanzania yeyote, angekuwa anamiliki moja ya nyumba zile je angeuza kwa bei ya hasara kiasi kile?
..ule ulikuwa ni WIZI na HUJUMA ya waziwazi. Cabinet ilikuwa inajua nini kinakwenda kutokea.
..Waziri mwenye dhamana na nyumba zile ambaye alipaswa kuupinga uamuzi huo naye akawa mstari wa mbele kutekeleza hujuma hiyo.
..sasa sijui kama unafahamu kwamba Dr.Kawambwa alipata kuliambia bunge kuwa serikali haikufikia lengo la mapato ililokuwa imejiwekea walipochukua uamuzi wa kuuza nyumba.
..Yaani hiyo ni hasara juu ya hasara.
..ni kweli ulaya, marekani, canada, etc wana programs za kuuzia WANANCHI WA KAWAIDA nyumba za bei nafuu.
..sijawahi kusikia wakina Bill Clinton, George Bush, Tony Blair, na wakubwa wa serikalini za nchi hizo wakisuka mipango ya kujitwalia assets za serikali zao kwa bei ya hasara.
..tena huko magharibi wakiwa na mpango wa kuuza nyumba kwa wananchi wa kawaida wasimamizi wa mpango huo hawaruhusiwi kununua nyumba hizo au kufaidika kwa namna yoyote ile.
..mwisho, hii nchi ina matatizo mengi sana. Sasa sitegemei serikali yetu ikauza assets zake kwa mtindo wa kihasara-hasara kama ilivyofanyika ktk kuuza nyumba za serikali.
..nyumba zile zingeuzwa kwa bei ya SOKO tungeweza kutatua baadhi ya matatizo yetu mfano ujenzi wa maabara, maktaba, madawati etc etc.