Na mimi ndivyo nilivyo adithiwa, wa lisema siku yenyewe ilikuwa ni Chrismas kama nakumbuka vizuri.
Inaelekea Dk. Kleruu (RIP) alipata taarifa kuhusu Mwamwindi kuwepo shambani kwake akiwa na wafanyakazi wake - nadhani mwaka huo ndio itikadi za ujamaa zilikuwa zimepamba moto nchini, mabepari wakawa wanafananishwa na wanyama,wakaitwa wanyonyaji, wanaibwa kwa nyimbo za kejeri na chuki - yaani wananchi walikuwa primed kuwaona mabepari kama ni wabaya kuliko wakoloni.
Misimamo ya kuchukia Ubepari nchini ilikuwa ina walakini sana, kuna baadhi ya wananchi waliokuwa na uwezo kifedha walipata wakati ngumu sana kwa kunyaganywa mali zao walizo chuma kwa jasho lao!!
Atittude zilizokuwa zimejengeka wakati huo ndizo zilimpa jeuri Dk.Kleruu kwenda kumudhihaki/dhalilisha Mr.Mwamwindi skiwa shambani kwake - kisa? Mwamwindi ni bepari, eye witness walisema walimuona Dk.Kleruu ameshikilia kifimbo akikisukuma sukuma kwenye tumbo la Mwamwindi - hakuna mwanamume worthy his salt angeweza kuvumilia provocation ya kiwango hicho - alicho kosea Mwamwindi ni kule kwenda kuchukua Rifle kutoka nyumbani kwake na kurudi shambani kumpiga risasi Dk.Kleruu - sasa time lag ya kutoka shambani kwenda nyumbani kuchukua bunduki na kurudi tena shambani hasira zilipashwa kuwa zimepungua ndio maana mahakama ilimuhukumu kunyongwa kutokana na kuonekana kwamba iliuua kwa kukusudia "murder case"
Ile ilikuwa sera yakutaifisha mali za waislamu wengi waliojaa mijini na vijijini hasa Dar, kumbuka huko maporini shinyanga na kigoma kulikuwa na simba na mafisi tu ndio wametawala. Mfano likaundwa shirika la nyumba ili kujimilikisha nyumba za waislamu waliowengi.
Kama Mwamwindi angekuwa na bunduki shambani alafu Dk.Kleruu akaja akamu-provoke hapo angehukumiwa kuua bila ya kukusudia akafungwa kwa muda.