Nyumba aliyoishi RC wa Iringa Dr. Kleruu kabla ya kuuawa na Said Mwamwindi

Nyumba aliyoishi RC wa Iringa Dr. Kleruu kabla ya kuuawa na Said Mwamwindi

Dr.Kleruu alipigwa Risasi Shambani kwa Mwamwindi akiwa Kaenda kumzuia asilime Mazao anayoyataka badala yake alime zao la biashara kwa Gharama zake halafu akawauzie vyama vya ushirika kwa bei waliyojipangia serikali halafu watalipa siku wakijiskia, hata Risasi alipigiwa shambani sio gesti wala kitandani.
Enzi zile ni enzi za Propaganda kama uliweza kuaminishwa Iddi Amin anakula watu na wewe ukaamini huwezi kuacha kuamini uongo eti kisa Kilikuwa uzinzi!
Nawe si umeaminishwa hayo na yule marehemu ustaadh ilunga?
 
Dr. Kleruu wapo wengi sana Nyakati hizi ila Majasiri kama akina Said Mwamwindi hawapo!!
Huyu Mkulima alimtandika Risasi RC akamtia kwny Trekta lake akampeleka kwa RPC akamwambia nimewaletea Mzoga Wenu.
Juzi kati hapa Mgambo tu wa TANAPA wameharibu mashamba ya Mahindi zaid ya heka 400 huko Mbeya kisa wamelima kwenye Hifadhi, halafu wanakijiji wanakimbilia ITV !!!
No, sio trekta.
 
Hawa akina Mwamwindi wapo sehem gani hapo Iringa.. tupay visit ...
The untold heroes.
 
Na Mwamwindi kilipata nini baada ya hapo?
CC . RC Mwanza..!
Alishinda kesi...lakini kutokana na kwamba viongozi wengi wanatabia kama zake
Mkuu akaona hapana
Ngoja wamtoe mfano ili kuwatisha wengine.
 
Ilikuweje aende peke yake bila mtu mwingineAyote, dereva, askari, mkuu wa Wilaya.

Unajua ni kwa nini wakuu wa mikoa waliandamana Ikulu baada ya hukumu ys awali?

Usikurupuke mkuu, kuna kitu zaidi ya hicho ulichoaminishwa
Mkuu hebu funguka, niliwahi kuwaukiza wenzangu same question why alienda mwenyewe? Why ali drive mwenyewe?
 
Siyo kweli! Mwamwindi aliua kwa vile alikuwa provoked na huyo RC. RC alimfuata shambani kwake akiwa anasimamia vibarua, shamba ambalo lilikuwa kubwa sana na wakati huo ndo siasa ya ujamaa na kujitegemea ilikuwa imeshika kasi, Mwamwindi wakawa wanamwona kama bepari fulani hivi. Maana jamaa alikuwa amejiimarisha sana katika maswala ya kilimo, ieleweke kwamba enzi hizo watu waliokuwa na combine harvester walikuwa wa kuhesabika na Mwamwindi akiwamo. RC alipofika shambani kwa Mhehe akawa anamchomachoma tumbo kwa fimbo yake (kama ya Nyerere) huku akisema hili tumbo lina mirija ya unyonyaji. Hapo hapo Mhehe akahamaki ndo akaenda kuchukua riffle yake na kummiminia risasi hapo hapo shambani. Wacha niishie hapo maana hadithi ya Mwamwindi ni ndefu sana! Wewe kijana wa jana nawe unajidai kutuletea hadithi ya Mwamwindi?

Mkuu upo sahihi kabisa na hiyo ishu mzee wangu aliishuhudia kwa macho yake, anasema ilikua 26 december boxing day na yeye alikua ni mmoja kati ya vijana wa wakulima wakubwa waliopelekwa detention baada ya hayo mauaji...babu yangu yeye aliwekwa detention Dodoma ila walikuja kuachiwa huru na Mwamwindi alinyongwa.
 
Tangu wamwue Mwamwindi, Isimani sasa hivi inapelekewa misaada ya chakula tofauti na enzi za hao wazee, ilikuwa na uwezo wa kulisha mikoa kadhaa ya Tanzania. Lukuvi yupo jina tu!
 
Vyovyote itakavyokuwa iwe ishu ya shamba au mke lakini huyu mzee alikuwa anapinga unyonyaji
 
Uoga upi wa kuishi nyumba hiyo? Alafu naona kama nyumba imetelekezwa kama gofu vile. Watenge bajeti waikarabati watumishi wa serikali wanahangaika na uhaba wa nyumba za umma
 
Dr Kleruu alikua Mtwara kabla ya kwenda Iringa na kwa stori ya dingi anasema hata huko Mtwara hakuondoka vizuri kutokana na tabia yake ya ubabe na dharau
 
Tangu wamwue Mwamwindi, Isimani sasa hivi inapelekewa misaada ya chakula tofauti na enzi za hao wazee, ilikuwa na uwezo wa kulisha mikoa kadhaa ya Tanzania. Lukuvi yupo jina tu!

Upo sahihi kabisa Isimani imekua kama jangwa nlipita kwa babu kijiji cha Matembo nikaoneshwa mashamba yake ya zamani ambayo yalitaifishwa enzi hizo yamebaki pori tuu
 
Tangu wamwue Mwamwindi, Isimani sasa hivi inapelekewa misaada ya chakula tofauti na enzi za hao wazee, ilikuwa na uwezo wa kulisha mikoa kadhaa ya Tanzania. Lukuvi yupo jina tu!

na kilimo kilikufa kabisa maana wakulima wote wakubwa waliwekwa kizuizini
 
nlibahatika kuona kaburi la huyu Mwamwindi pia nlifika eneo alipopigwa risasi mkuu wa mkoa...si mbali sana toka iringa mjini njia kuu ya kwenda Dodoma ni mwendo wa dakika 40 kwa basi yaan ni barabarani kbs kama mita 20 hvi toka barabara kuu kuna mnara.
Nilikutana na mzee mmoja akanisimulia kifupi kuwa chanzo hasa ni mkuu wa mkoa kutaka Mwamwindi akawe eneo lake kwa baadhi ya wanakijiji maana mwamwindi alikuwa na mashamba makubwa sana lkn mwamwindi alikataa akadai lile shamba aliloliendeleza hatotoa kwa mtu labda atoe pori wafyeka wao. Mkuu wa mkoa kwa dharau na kibur akawa analazimisha...ulikuwa ni msuguano wa muda mrefu sana baina ya mkuu wa mkoa na wakulima wakubwa wa isimani enzi hizo mpaka siku ya tukio jamaa alimfuata shamba akiwa peke yake hii inaonyesha jinsi mkuu wa mkoa alivyokuwa na dharau kuwa hakuna wa kumtisha . Jaman wahehe hawapendi kudharauliwa hasa hasa mbele ya mke au/na watoto ataua aisee....ukisikia mhehe amesema SWELAGA HELAA akiwa amekasilika basi hapo ni kuua au kujiua tu na ndicho alichokifanya Mwamwindi,ajabu mkuu wa mkoa aliendeleza dharau kwa vijana na mke wa mwamwindi waliokuwepo shamban siku hyo,mzeee akaenda kuchukua bunduki
ni stori ndefu
 
Dr. Kleruu wapo wengi sana Nyakati hizi ila Majasiri kama akina Said Mwamwindi hawapo!!
Huyu Mkulima alimtandika Risasi RC akamtia kwny Trekta lake akampeleka kwa RPC akamwambia nimewaletea Mzoga Wenu.
Juzi kati hapa Mgambo tu wa TANAPA wameharibu mashamba ya Mahindi zaid ya heka 400 huko Mbeya kisa wamelima kwenye Hifadhi, halafu wanakijiji wanakimbilia ITV !!!
Siyo kwenye tractor mkuu, aliuweka mwili wake kwenye gari ya serikali Peugeot 404 aliyokuwa anatumia RC akaendesha yeye hadi central police huku pia akiwa amevaa kofia - pama ya marehemu
 
Munyalukolo mwamwindi akakamata riffle akasema this my riffle, this my gun, tis for fighting, this for fun. Akamtandika Dr kleruu akarest in peace.......
 
Back
Top Bottom