Nyumba aliyoishi RC wa Iringa Dr. Kleruu kabla ya kuuawa na Said Mwamwindi

Nyumba aliyoishi RC wa Iringa Dr. Kleruu kabla ya kuuawa na Said Mwamwindi

Kawaida sana Raisi wa Brazil alikuwa analalamika ikulu yake ina mambo ya abrakadabra wangemsikiliza ingewabidi wajenge ikulu nyingine sasa ije kuwa hii ya DC!😀...
 
Hii ni nyumba ya kihistoria iliyojengwa na muingereza ambayo baada Tanzania kupata uhuru nyumba hiyo ilianza kutumiwa na Mkuu wa mkoa ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mmoja wa wasomi wachache waliokuwa Tanzania ndugu Dr. Wilbert Kleruu.

Kwa wale wanaoijua historia na wale waliosoma sheria jina Said Mwamwindi na Dr. Kleruu (Said Mwamwindi v R (1972) HCD 212 ) sio majina mageni kwao.Pia kuna chuo cha Ualimu kimejengwa kuenzi kazi iliyotukuka ya Dr. Kleruu.

Kwa bahati mbaya nyumba hii haijatumiwa tena na wakuu wa mikoa waliofuata baada ya kifo cha Dr. Kleruu kutokana na kile kinachosemekana kuwa uoga.Nyumba hii imekuwa ikitumiwa na Jeshi.

Mbaraka Mwinshehe naye amepata kumuimba dr. Kleruu
Hivi itahidi kuta picha ya Dk Kleru sijafanikiwa nani anaweza kunisaidia??
 
Ilikuweje aende peke yake bila mtu mwingine yeyote, dereva, askari, mkuu wa Wilaya.

Unajua ni kwa nini wakuu wa mikoa waliandamana Ikulu baada ya hukumu ys awali?

Usikurupuke mkuu, kuna kitu zaidi ya hicho ulichoaminishwa
Mmmmmmh mbona naanza kupata wasiwasi na hii historia? isije kuwa ilishachakachuliwa na kuaminishwa ndivyo sivyo. Coz sisi ni mabingwa wa propaganda balaaa(Kama tulivyoaminishwa kuwa Iddi Amini alikuwa anakula nyama za watu😡😡😡)
 
JIBU ZURI UNAPANGIWAJE ZAO LA KULIMA KAMA VP SI ALIME MWENYEWE alaaa waleta upumbavu hapa
 
Huyo Mwamindi akahukumiwa kunyongwa, akafa akazikwa. Familia yake ndiyo iliyopata tabu kwa kuondokewa na baba kwa sababu za kipumbavu. Afadhali angemchapa makofi Kleruu ingeeleweka anatetea uanaume wake mbele ya umma. Binafsi nauchukia sana ujamaa kwa kuwa ni uonevu mkubwa na unalea uvivu. Lakini ninyi mnaotetea fujo naamini hamjawahi kushuhudia vita au kuishi kwenye nchi za vita. Msiombee. Kuna viongozi wa serikali wanaongea na kufanya maudhi kupata kiki lakini msihamasishe fujo. Hapatakalika.
 
Hata Said Mwamwindi 'kosa lake' ni kulima zao lisilotakiwa kulimwa lakin hakukimbilia 'ITV' matokeo yake alitafakari akachukua Hatua
Alikuwa mzinzi sana, acha ubishi....
 
Imefika wakati haya mambo yakawekwa wazi kwenye vitabu. Hii nchi inapotezwa sana na wanasiasa, wakifuatiwa na wasomi ambao wamegeuka wanafiki na waabudu sanamu za wanasiasa. Unawakuta wasomi hasa, hadi anaitwa profesa au dr lakini wamebaki wanafikiri hivyo vyeo wamewewa kwa lengo la kwenda kujitafutia rizki na kushibisha tumbo hata kwa kuabudu na kukariri ngonjera za kisiasa. Vyeo vya Dr au Prof ni pamoja na mental independence na kubaki kwenye fact hata kama kuna kifo mbele yako.
 
Hii ni nyumba ya kihistoria iliyojengwa na muingereza ambayo baada Tanzania kupata uhuru nyumba hiyo ilianza kutumiwa na Mkuu wa mkoa ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mmoja wa wasomi wachache waliokuwa Tanzania ndugu Dr. Wilbert Kleruu.

Kwa wale wanaoijua historia na wale waliosoma sheria jina Said Mwamwindi na Dr. Kleruu (Said Mwamwindi v R (1972) HCD 212 ) sio majina mageni kwao.Pia kuna chuo cha Ualimu kimejengwa kuenzi kazi iliyotukuka ya Dr. Kleruu.

Kwa bahati mbaya nyumba hii haijatumiwa tena na wakuu wa mikoa waliofuata baada ya kifo cha Dr. Kleruu kutokana na kile kinachosemekana kuwa uoga.Nyumba hii imekuwa ikitumiwa na Jeshi.

Mbaraka Mwinshehe naye amepata kumuimba dr. Kleruu
Hivi Tanzania ilipata uhuru lini?
 
Ni kweli, Dr. Kleruu hakuwa na ethics. Siku hiyo ya krismas aliyokumbwa na mauti aliondoka kwenda kumchukua yule mwanamke wa mzee Mwamwindi bila hata kuwa na dereva wala askari mlinzi. Kwa bahati mbaya alipofika pale akamkuta mzee Mwamwindi mwenye mali mwenyewe akiwa yupo nyumbani. Yaliyobaki leo ni historia tu.
Wewe ndio umesema historia halisi, hawa wengine wanapotosha tu. Watanzania bwana sijui nani alituroga tu? Hivi kuna haja gani ya kupindisha pindisha historia> Dr. Kleruu alikua mzinzi kama yalivyo ma ccm menzake leo hii, na kwa kweli alilipwa sawa sawa kutokana na matendo yake. Huo ndio ukweli, na Vijana wangu hiyo ndiyo historia ya kweli. Msipotoshwe.
 
Back
Top Bottom