Nyumba anayodai Polepole imevunjwa siyo makazi yake ya kibunge, analaghai Umma akishirikiana na aliowakuza awamu iliyopita

Nyumba anayodai Polepole imevunjwa siyo makazi yake ya kibunge, analaghai Umma akishirikiana na aliowakuza awamu iliyopita

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Polepole anatafuta namna ya kuwafanya Wananchi wajinga, anatafuta namna ya kutumia kile chumba anachodai kimevunjwa kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni mzalendo na hakujilimbikizia Mali, anataka kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni fukara na mtu wa kiwango Cha chini kimaisha. Tumpuuze

Kwanini ameyafanya haya? Kwanza anataka kubadili upepo na agenda za kitaifa ikiwemo katiba Mpya na kutamka kurejea kwenye meza ya mazungumzo ndani ya CCM akionekana mwanamikakati. Hii tabia ya miaka mingi inayotumiwa na walafi wa madaraka.

Pili anataka yeye pamoja na vibaraka wake endapo mfumo utaamua kufungua shauri na kuchunguza MATENDO yake ndani ya chama na adhari zake kwenye serikali basi arudi Kwa Wananchi kupitia picha alizotuma apate uungwaji MKONO kwamba anaonewa. Mfano mzuri WA eneo analojua linaweza kumpeleka mahakamani kwa makosa ya Uhujumu uchumi ni pamoja na kununua wapinzani ambapo mfano wa wazi ni kile kitendo Cha yeye kupeleka milioni 30 mahakamani kumnunua Mashinji.

Tatu, kupitia tukio hili anataka kunyamaza atuaminishe amenyamazishwa kumbe maovu yake huko nyuma yalishamnyamazisha Toka mteule wake wa awali alipoondoka.

Polepole amekuwa live kwenye shule yake sijui ya siasa na mandhari aliyokuwa anarushia matangazo ipo wazi, anamzuga Nani? Wabunge Wana nyumba Dodoma yeye alikwenda kupanga chumba Kwa kukosa Kodi au kwa sababu gani? Mbunge Hana viti Wala kitanda, hizi michezo inatuondoaje kwenye reli? Lakini pia kaongea Dar mara kesho yake anadai alikuwa Manyara na anarudi Dodoma ndo anakuta pamevunjwa je Hana majirani? Hawa watu wanapeana michongo ya kututawala Kwa kupanua magoli , tushtuke uhuni huu.
 
Acheni ujinga wenu hapa. Hamuwezi kujadili masual ya maana, angalau namna ya kuinua maisha na mifumo badala ya majungu yenu ya kipumbavu? We are tired of you idiots. Kwa nini hamkusema habari hizi wakati akiwa bado yuko akpiga makofi ya kipumbavu?
 
Nyumba ya Polepole kuvunjwa haijalishi iwe ya kibunge au ya kiraia huo ni uhalifu na unatakiwa kufanyiwa kazi na jeshi la polisi bila kujali chochote.

Kusema Polepole anajikweza kisa nyumba yake haikuwa na mali nao ni ushamba tu, ingekuwa na mali nyingi naamini pia ungesema Polepole fisadi, kuwa na mali nyingi au chache ni life style ya mtu yeyote anajiamulia, sio kigezo cha uzalendo, na sio kila mwenye mali nyingi au chache ni mwizi au mtakatifu, hizi sababu nyepesi ulizo leta hapa hazina mashiko.

Kuhusu majirani sidhani kama Polepole ameajiri majirani zake wawe walinzi wake, nao wanakazi zao, una hakika wakati wa tukio hao majirani walikuwepo nyumbani? na kama walikuwepo hawakuwa na shughuli nyingine wakawa wametega macho na masikio yao kwa Polepole tu?

"Ushuani" ni tofauti na "uswahilini" ambapo kila anaeingia na kutoka huonekana, hata ukila maharage kwako majirani wote wanajua, usikariri maisha yako ukayahamishia kwa mwenzako.

Siku hizi watu wanapanda ndege wanazunguka karibia nchi nzima kwa siku moja, wewe unashangaa umbali kati ya Manyara na Dodoma ambao hata kwa gari mtu anafika? hizi mindset zenu.

Hicho kikao walichokaa Polepole na CCM wenzake ili watuondoe kwenye lengo la msingi [Katiba Mpya] kilifanyika lini na wapi? Kila siku mnalilia mikutano ya kisiasa irudishwe kwa wote, ila Polepole kutoa maoni yake apuuzwe!, hamkumbuki anayemnyima Polepole ndie anaewanyima nyie.

Sio kwasababu Polepole ni mwanasiasa mwenye mawazo tofauti na kambi yake ndio aanze kutengwa na kutafutiwa sababu za kila aina, ajibiwe hoja zake maisha yaendelee, kwasababu ni haki yake kutoa maoni na wanaoulizwa sharti wamjibu wasimtishe, kumkejeli, au vyovyote vingine.

Haiwezekani leo kutaka Polepole apuuzwe kwa kutoa hoja zake, ila nyie "wana demokrasia" mkitoa hoja zenu mtake zijibiwe, hii ni double standard, haki haina mipaka na haichagui sura, kama mnaona Polepole ana makosa nendeni mahakamani na hao wenzenu mliowaunga mkono bila kujitambua, opposition is an art.
 
Pole pole anatafuta namna yakuwafanya Wananchi wajinga, anatafuta namna yakutumia kile chumba anachodai kimevunjwa kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni mzalendo na akujilimbikizia Mali, anataka kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni fukara na mtu...
Kuna Watu Walitoa Cctv Kabla Ya Lissu Kushambuliwa Kwenye Utawala Dhalimu Wa Ccm Hakuna Kinacho Shindikana;

Pole Pole Anapitia Maumivu Waliyopitia Wenzie Enzi Zile Yeye Akiwa Kwenye V8;
 
Ama kweli hii ni JF mpya...nimetafuta like nilichokiona kwenye Heading sijakiona kabisa kwenye COntent!
Halafu kumbe Wabunge Wana Makazi ya Kibunge Dodoma...!?
Anyway huu ni Utopolo tu.
Ukweli unabaki palepale tatizo ni CCM
 
Nyumba ya Polepole kuvunjwa haijalishi iwe ya kibunge au ya kiraia huo ni uhalifu na unatakiwa kufanyiwa kazi na jeshi la polisi bila kujali chochote.

Kusema Polepole anajikweza kisa nyumba yake haikuwa na mali nao ni ushamba tu, ingekuwa na mali nyingi naamini pia ungesema Polepole fisadi, kuwa na mali nyingi au chache...
Uko biased..kumbe wewe umesmamia itikadi yako bali sio Ukweli wa kile akisemacho Pole Pole.
 
Polepole anatafuta namna ya kuwafanya Wananchi wajinga, anatafuta namna ya kutumia kile chumba anachodai kimevunjwa kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni mzalendo na hakujilimbikizia Mali, anataka kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni fukara na mtu wa kiwango Cha chini kimaisha...
Mumy Naona hujapata cha asubuhi, ukishapata twambie
 
Katika Hii ya Polepole upinzani umeingia mkenge,kuungana na CCM kumpinga Polepole.

Jana Star TV kwenye kipindi Cha "The big Agenda" John Heche alijiunga na mbunge wa CCM (nimesahau Jina)kumpiga vijembe Polepole!

Chadema wajichunge wasitolewe kwenye reli na CCM kwa hizi issue za Polepole.

Jamaa huenda yupo kimkakati!
 
Polepole anatafuta namna ya kuwafanya Wananchi wajinga, anatafuta namna ya kutumia kile chumba anachodai kimevunjwa kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni mzalendo na hakujilimbikizia Mali, anataka kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni fukara na mtu wa kiwango Cha chini kimaisha. Tumpuuze....
Hayo ni mawazo yako
 
Polepole anatafuta namna ya kuwafanya Wananchi wajinga, anatafuta namna ya kutumia kile chumba anachodai kimevunjwa kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni mzalendo na hakujilimbikizia Mali, anataka kuonyesha Wananchi kwamba yeye ni fukara na mtu wa kiwango Cha chini kimaisha. Tumpuuze....
Majiran wepi wasikie kwako kunavunjwa watoke mzee unaonekana mgeni na Tanzania panya road wanakaba hapa watu wanapita pemben
 
Nyumba ya Polepole kuvunjwa haijalishi iwe ya kibunge au ya kiraia huo ni uhalifu na unatakiwa kufanyiwa kazi na jeshi la polisi bila kujali chochot
Huyu mtoa post huwa simwelewi kabisa. Hajulikani anachotaka ni kipi hasa. Post zake nyingi umbeya tu na utoto
 
Nyumba ya Polepole kuvunjwa haijalishi iwe ya kibunge au ya kiraia huo ni uhalifu na unatakiwa kufanyiwa kazi na jeshi la polisi bila kujali chochote...
Tuna matukioo mengi ya kuchunguza kabla ya kuchunguza Hilo la polepole.

kuna watu wamepitia maumivu makubwa kuliko yeye.

na yeye akatafuta vijana mitandaoni wa kuitetea CCM.

Mara ngapi zimeandikwa mada kuwa Ben saa 8 amejiteka?

watu wameteseka Sana kwa ajili ya UONGOZI wao mbaya.

leo anataka kuongea nini?

"MNASAHAU MAPEMA SANA"
 
Back
Top Bottom