Nyumba, Duka vinauzwa na NMB Bank

Nyumba, Duka vinauzwa na NMB Bank

Ni kweli mkuu, hata mimi nilikuwa najifanya msomi saana, kila aliyekuwa ananiambia habari kama hizi nilimuona mjinga na punguani, hata habari za mila nilikuwa naona ni ujinga mtupu mkuu.

Ukisema watu wengi nakuelewa kabisa, kila nyumba inayouzwa iliyokopewa ina simulizi yake na hali yake ya kipekee. Nakiri pia sio zote. Wengine huwa wanakopa na hawalipi makusudi ili nyumba iuzwe, na wengine ni waelewa, wanajua madhara ya kutokulipa deni.

Acha uongo Mkuu.

Hizo ni hadithi tuu za kubuni zinazoaminiwa na Watu wenye upeo mdogo
 
Usithubutu kununua!! Utarogwa kuna jamaa yangu yupo mikoa ya kusini, alijaribu kununua nyumba ya namna hiyo, bado kdg roho ichomoke, watu wakamstua kuwa huku wazee wakikopa, na benki wakatangaza mnada, huwa hawajitokezi maana mwenye mali anaweka uchawi kwenye hizo mali, ye alikuwa mgeni na hela zake uhamisho hajui hili na lile, akaenda kwenye mnada, almanusura roho ichomoke na bahati yake alipozinduka hospital, yule mzee alimuibukia akamwambia pole sana kumbe we u mgeni? Basi utapona ukaendelee na maisha yako, ila usikurupuke kununua vitu vya madeni na madai

Hizo ni hadithi za Uongo.
Hakuna kitu kama hicho.

Nina ndugu kibao wamenunua nyumba mikoa Lindi na mtwara na wanaishi vizuri licha ya kuwa walitishiwa kwa maneno na wajinga wanaoamini vitu vya kipuuzi kama wewe
 
Lakini Mkuu kumbuka kuna nyumba mtu anakopea Bank kwa makusudi kabisa akiwa kadhamiria kutolipa mkopo huo.Mara nyingi unakuta thamani ya nyumba ilikuwa inflated kuliko uhalisia na mtu anachukua mkopo mkubwa kuliko thamani ya nyumba.Hizo ukiuziwa hazina shida.

Kuna hizi ambazo waliokopa walikuwa na nia ya dhati ya kulipa lakini wakashindwa na nyumba ikauzwa huku wanalia machozi.Hizi ni za kuogopa sana kuzinunua.

Hata wangelia machozi ya Damu hakuna kitakachoweza kutokea.
Hawakutumwa Wakope.

Acheni imani potofu
 

Raha ya humu mitandaoni si hatujuani mkuu, huwa tunajifanya hatuna imani kabisa na mambo ya mazingaombwe, hatuamini uchawi. Ogopa sana unanunua nyumba kwenye mnada na mwenye nyumba yake yupo hapo machozi yanamtoka.

Kwa mliopo mjini Dar, kuna nyumba kadhaa tu zimetelekezwa, watu hawakai!

Nitafutie hiyo nyumba iliyotelekezwa alafu nije nikae.
Haifurahishi mwanaume kuwa na mawazo kama haya
 
Hiyo changamoto huwa inatokea mara moja moja. Na kamwe haiwezi kuwakatisha tamaa wafanyabiashara. Maana faida ya hiyo mikopo kwa mtazamo wangu, naona ni kubwa zaidi kuliko hasara.
 
Back
Top Bottom