Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
kama wewe unavyomtangaza.......Nimejifunza kitu hapa, Nmb wakipita kuhamasisha mikopo wapole kweli.
Ukishindwa kurejesha wanakutangaza na vipaza sauti mitaa yote.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kama wewe unavyomtangaza.......Nimejifunza kitu hapa, Nmb wakipita kuhamasisha mikopo wapole kweli.
Ukishindwa kurejesha wanakutangaza na vipaza sauti mitaa yote.
Ni kweli mkuu, hata mimi nilikuwa najifanya msomi saana, kila aliyekuwa ananiambia habari kama hizi nilimuona mjinga na punguani, hata habari za mila nilikuwa naona ni ujinga mtupu mkuu.
Ukisema watu wengi nakuelewa kabisa, kila nyumba inayouzwa iliyokopewa ina simulizi yake na hali yake ya kipekee. Nakiri pia sio zote. Wengine huwa wanakopa na hawalipi makusudi ili nyumba iuzwe, na wengine ni waelewa, wanajua madhara ya kutokulipa deni.
Usithubutu kununua!! Utarogwa kuna jamaa yangu yupo mikoa ya kusini, alijaribu kununua nyumba ya namna hiyo, bado kdg roho ichomoke, watu wakamstua kuwa huku wazee wakikopa, na benki wakatangaza mnada, huwa hawajitokezi maana mwenye mali anaweka uchawi kwenye hizo mali, ye alikuwa mgeni na hela zake uhamisho hajui hili na lile, akaenda kwenye mnada, almanusura roho ichomoke na bahati yake alipozinduka hospital, yule mzee alimuibukia akamwambia pole sana kumbe we u mgeni? Basi utapona ukaendelee na maisha yako, ila usikurupuke kununua vitu vya madeni na madai
Lakini Mkuu kumbuka kuna nyumba mtu anakopea Bank kwa makusudi kabisa akiwa kadhamiria kutolipa mkopo huo.Mara nyingi unakuta thamani ya nyumba ilikuwa inflated kuliko uhalisia na mtu anachukua mkopo mkubwa kuliko thamani ya nyumba.Hizo ukiuziwa hazina shida.
Kuna hizi ambazo waliokopa walikuwa na nia ya dhati ya kulipa lakini wakashindwa na nyumba ikauzwa huku wanalia machozi.Hizi ni za kuogopa sana kuzinunua.
Acha uongo Mkuu.
Hizo ni hadithi tuu za kubuni zinazoaminiwa na Watu wenye upeo mdogo
Raha ya humu mitandaoni si hatujuani mkuu, huwa tunajifanya hatuna imani kabisa na mambo ya mazingaombwe, hatuamini uchawi. Ogopa sana unanunua nyumba kwenye mnada na mwenye nyumba yake yupo hapo machozi yanamtoka.
Kwa mliopo mjini Dar, kuna nyumba kadhaa tu zimetelekezwa, watu hawakai!
Kabisa mkuu!
Usiamini vitu vya kipuuzi.
Ushakua mtu mzima sasa. Tena ni mwanaume.
Sawa mkuu!