Nyumba kama hii inaweza kuuzwa bei gani?

Nyumba kama hii inaweza kuuzwa bei gani?

Nahitaji kujua tathmini ya kuuza nyumba hii. Ina vyumba 2 na sebule pamoja na jiko, master bedroom ni self, chini Kuna tiles na juu Kuna gypsum board pia imepigwa rangi za kisasa ndani na nje na dirisha zote ni aluminum.

Msaada tafadhali.

View attachment 1981494
Inategemea na ukubwa wa kiwanja hali ya kiwanja na miundombinu pamoja na location.

Hapo ni kati ya 12M-18M
 
Inategemea na location ilipo, but ni almost 25-30 kulingana na sehemu ilipo
 
Bei ya nyumba inategemea vitu vikuu vitatu:-

1. Miundombinu eg Barabara,Maji,Umeme,surveyed etc
2.Muonekano/Ubora eg Ya kisasa,Ghorofa,Pagale,iliyopangwa tofali
3.Location eg Dar ,Arusha ,Masaki ,Oysterbay ,Manerumango ,Mpitimbwi etc
Umesahau ukubwa wa kiwanja
 
Sasa uliyejenga nyumba unatuuliza sisi tukushauri bei. Ninachofahamu kuuza nyumba mtu anapiga gharama zake zote kuanzia kiwanja mpaka mwisho. Kisha angalia wakati, Kama ulijenga miaka 5 nyuma je thamani ya fedha leo ikoje? Wakati utaamua kiwango cha faida au hasara utakayopata.
 
Back
Top Bottom