Nyumba kigogo Mbuyuni Dar es Salaam kubomolewa

Pole sana...
Mleta mada fuata miongozo hiyo....
 
Wapo kwenye eneo la mradi na ukizingatia kuwa wana kitega uchumi chenye thamani kubwa na ili uwaondoe inahitajika pesa ndefu sana,hivyo wanahitaji fidia ya ardhi na si ardhi ndogo na ndo maana lazima waingizwe kwenye mpango
Huyu Fida Hussain ni yule mwenye apartments kibao pale nyuma ya TMJ hospital??
 
Nakwambia tena World Bank huwa haitoi compensation kwenye miradi yake refer Barabara ya Kimara-Kibaha, na miradi mingine mingi naifahamu ni serikali ndiyo huwa inatoa fidia na ikigoma wao husitisha kutekeleza mradi
Exactly [emoji1666][emoji1666]
 
Ni kote hadi huku kinondoni Hananasifu. Watu wa world Bank wanafanya mikutano na wenye nyumba wanasema watalipa vizuri tu hadi ya usumbufu.
 
Kwa hapo TMJ sifahamu ila miongoni mwa nyumba anazomiliki Fida ni zile pale nyuma ya Tanesco Mikocheni
Atakuwa amechanganya ila ndio izoizi upande wa pili baada ya Tmj
 
Ok ndio maana huku bonde la msimbazi upande wa mchikichini baadhi ya nyumba zimeandikwa kwa namba rangi kijani ndio wanaanzia wao kufanyiwa tathimni,na wale walioandikiwa na namba kwa rangi nyekundu wameambiwa wasubiri,sasa hapo inamaana hawa waliandikiwa rangi nyekundu kunauwezekano wa wao kubaki maeneo hayo sio
 
Mama yangu bint Musa anakibanda pale kigogo Ruhanga kwa bint Kaenga aliwahi nihadithia hii stori miaka miingi nyuma nadhani ndo linatimia.
Alisema nyumba zitavunjwa na kujengwa ghorofa na mwenye kiwanja ataishi umo umo.
Wakati ananiadithia sikulichukulia kwa uzito
 
Mwenyekiti wa Serikali za mtaa na wajumbe wake wanasemaje? Hao lazima wawe na majibu sahihi
 
JFs ina taarifa nyingi aisee
 
Wanajengewa apartment wakae pamoja waache kusambaaaa bonde zima. Eneo kinalobaki wanachukua Mabwanyenye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…