Nyumba moja kuwa na meter kumi za LUKU haina maana, Napendekeza LUKU moja iwe na line nyingi kama simu

Nyumba moja kuwa na meter kumi za LUKU haina maana, Napendekeza LUKU moja iwe na line nyingi kama simu

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Ni kwamba meter moja ya umeme iwe na uwezo wa kulisha nyumba hadi 6 bila kuchangiana kwenye matumizi.

Mteja akiomba meter, atasema anataka yenye output ngapi (line 1, 2 ,3, 4, 5 au 6) kulingana na matarajio yake ya kuongeza matumizi ya wapangaji au fremu za maduka baadae.

Kwahiyo meter itapokea wire mmoja wa umeme toka kwenye nguzo (Live na neutral), kisha kwenye out put utatoka wire mmoja tu wa neutral ambao utaenda kwenye nyumba zote (branching) zinazotaka kugawana umeme, halafu kutakuwa na wira kadhaa (mfano 6) za live ambazo zitaenda kwenye kila nyumba inayofanyiwa separation, ambapo kila wire ya live itakuwa na ‘Circuitry’ yake inayojitegemea ndani ya meter.

Kwahiyo wapangaji wote 6 wakitaka kununua umeme, wataingiza namba ile ile ya meter, ila tu mbele wataweka (/1) , (/2) , (/3) nk. kulingana na nyumba yake imechukua umeme toka kwenye output ya kwanza, pili, tatu nk. , hivyo akilipa umeme utaenda kwenye nyumba yake tu na sio zingine. Pia kwa kuongeza, mtu akinunua umeme, meter ijiwashe automaatic kama king’amuzi bila kuingiza tokeni.

Faida kuu: Badala ya kutumia milioni 2 kufunga meter 6 , sasa utatumia laki 3 na ishirini tu.
———————————————————-
Pia itaondoa multiple taxation ya kodi ya majengo ambapo nyumba moja hulipiwa kodi ya majengo na kila meter, hata kama zipo 10.
TANESCO
 
Nadhan serikali hufanya mambo yao kwa mipango kuliko unavyowaza wewe!

Kubadili luku nchi nzima kuna hitaji bajeti!

Pia kwasasa hao jamaa wanafunga smart meter! Pia kwa umeme wetu sishauri sana kuwa na Dual meter kwasasa fault ni nyingi sana!

Wayaring katika nyumba nyingi haziko sawasawa sana ..hivyo zikiletwa hizo dual meter haziwezi kuhimili mikiki ya umeme wetu mtakuja kuwalaum emergency bure tu!. Kuhusu gharama inaweza kuwa ndogo lakini changamoto zikawa nyingi kufanya replacement ya wingi wa mita zitakazokuwa zinaharibika kama simu za kichina.

Haya ni maoni yangu tu lakini kama fundi umeme samico 0711756341
 
Una maoni lakini kuwaona wenzako wajinga siyo pouw!
Nazan serikali hufanya mambo yao kwa mipango kuliko unavyowaza wewe...
Nani kasema wabadikishe hizi zilizopo, nimesema endapo mtu ataomba meter kwa kipindi kijacho, mfumo uwe ni huo, kwa ambao wanazo za njia moja waendelee tu kutumia kwani zina tatizo gani hadi zibadilishwe?

Pia hizo smart meter zionhezwe njia za output, nini kigumu hapo kwani kuelewa?
 
Ni kwamba meter moja ya umeme iwe na uwezo wa kulisha nyumba hadi 6 bila kuchangiana kwenye matumizi.

Mteja akiomba meter, atasema anataka yenye output ngapi (line 1, 2 ,3, 4, 5 au 6) kulingana na matarajio yake ya kuongeza matumizi ya wapangaji au fremu za maduka baadae...
una mtazamo, maoni na mawazo mazuri sana ili ghadhabu na mihemko haikua na ulazima wowote kwenye heading ya bandiko lako 🐒

ustaarabu na staha katika matumizi ya lugha za kiungwana kwenye masuala muhimu kama hili, huvutia na kuongeza maana na umuhimu wa wazo lako, hata kufanyiwa kazi kwa haraka zaid na wahusika kuliko hivyo ilivyo sasa 🐒

Otherwise,
well and good...

Good idea but wrong presentation🐒
 
Unakwamisha maendeleo ya taifa? Lazima kuna pahali unafaidi wewe. Wala siyo bure!
Nimeshauri tu mkuu! Maendeleo ya nchi hii ni kupata umeme wa uhakika! Hivi vitu vingine siyo kipaumbele sana kwa sasa! Kuna faida gani kuwa simu ya laini nyingi kama simu haikai na chaji?
Tuishauri serikali wawe na uhakika wa chaji ndipo tuongelee mengine
 
Pia itaondoa multiple taxation ya kodi ya majengo ambapo nyumba moja hulipiwa kodi ya majengo na kila meter, hata kama zipo 10.
 
Cha kushangaza, nimejaribu kutafuta online kama kuna meter za line nyingi kama zinatengenezwa nchini China au kwingineko sijaziona kabisa, ugumu wake ni nini hasa kiasi hadi leo hazipo available kwenye market?
 
Back
Top Bottom