Nyumba moja kuwa na meter kumi za LUKU haina maana, Napendekeza LUKU moja iwe na line nyingi kama simu

Nyumba moja kuwa na meter kumi za LUKU haina maana, Napendekeza LUKU moja iwe na line nyingi kama simu

Watanzania kwa kuendekeza na kupenda anasa kwa kupenda umeme wakati kuna jua na mwezi unawaka kila siku. Mbona mababu zetu waliishi bila umeme na walikuwa na furaha tu na maisha yakaenda?
We mzee ha ha ha
 
Cha kushangaza, nimejaribu kutafuta online kama kuna meter za line nyingi kama zinatengenezwa nchini China au kwingineko sijaziona kabisa, ugumu wake ni nini hasa kiasi hadi leo hazipo available kwenye market?
bora hata ume google ukaona hakuna viability hapo
kwa haraka haraka, limita litakuwa likubwa, maana kila njia ndani ya mita inabidi iwe na PT, L-CT,N-CT, Relay yake
watakacho share vitu vidogo sana
 
Swala ni uaminifu, kila mtu aorotheshe vitu vyote vinavyotumia umeme na Watts zake, anatumia kwa mda gani , alipe kulingana na matumizi. Nyumba itatulia bila malumbano.
 
Nadhan serikali hufanya mambo yao kwa mipango kuliko unavyowaza wewe!

Kubadili luku nchi nzima kuna hitaji bajeti!

Pia kwasasa hao jamaa wanafunga smart meter! Pia kwa umeme wetu sishauri sana kuwa na Dual meter kwasasa fault ni nyingi sana!

Wayaring katika nyumba nyingi haziko sawasawa sana ..hivyo zikiletwa hizo dual meter haziwezi kuhimili mikiki ya umeme wetu mtakuja kuwalaum emergency bure tu!. Kuhusu gharama inaweza kuwa ndogo lakini changamoto zikawa nyingi kufanya replacement ya wingi wa mita zitakazokuwa zinaharibika kama simu za kichina.

Haya ni maoni yangu tu lakini kama fundi umeme samico 0711756341
GHARAMA ZA MITA TUNAWEZA KUZIONDOA KWA KUANZA KUTUMIWA KWA MITA HIZI KWA WATEJA WAPYA NA KUBADILISHA MITA MBOVU.
 
Watanzania kwa kuendekeza na kupenda anasa kwa kupenda umeme wakati kuna jua na mwezi unawaka kila siku. Mbona mababu zetu waliishi bila umeme na walikuwa na furaha tu na maisha yakaenda?
Umeme ni uchumi,umeme ni usalama,ni maendeleo na sioni chochote cha faida bila umeme!
 
Cha kushangaza, nimejaribu kutafuta online kama kuna meter za line nyingi kama zinatengenezwa nchini China au kwingineko sijaziona kabisa, ugumu wake ni nini hasa kiasi hadi leo hazipo available kwenye market?
MITA KUUNGUA KWA MZIGO MKUBWA KWA MITA MOJA(OVERLOAD).
 
Back
Top Bottom