Huu mtindo wa Biashara ni unaitwa Jenga Uza,ikimaanisha nyumba inajengwa kwa dhumuni la kuuzwa.
Huu mtindo unatumika sana wilaya ya Ilala : Homboza,Zingiziwa,Mvuti,Chanika,Msongola,Buyuni,Majohe na Pugu Kajiungeni.
Pia upo wilaya ya temeke:Mbande,Mbagala,Chamazi
*Sifa za huu ujenzi
1.Ujenzi huwa wa haraka:ndani wiki mbili nyumba inakuwa ishakamilika.
2.Bei nafuu;Kuna nyumba mpaka za millioni 15
*Ubovu wa hizi nyumba
1.Hutumia mchanga wa kiwango kibovu, nishaona huko Viwege wakitumia mchanga ambao unatoka kwenye chimbo asili ya maji chumvi, ukuta utarika na chumvi
2.Msingi jengo hawaweki zege la kuzunguka jengo, kama wakiweka wanalaza hata nondo moja.
3.Msingi kuwa mfupi kwenda chini:unakuta imelazwa kozi mbili tu ,wakati wanajua fikia hayo maeneo tajwa yana mchanga mwingi, inatakiwa angalau kozi tatu kwenda chini.
4.Masaa machche baada ya kujenga msingi kuta husimamishwa ;kwa maeneo kama haya ambayo yana mchanga wenye kupitisha maji kwa chini, angalau uwe unapumzika siku ili nyumba ishuke taratibu.
5.Matofali mabovu: matofali ya uwiano mbovu wa mchanga kwa simenti
6.Simenti ubora mdogo : simenti kama ya Camel
7.Hakuna upozaji wa joto la kuta wala plasta,,yani ukuta umejengwa leo,na beam zake, kesho plasta, kesho kutwa skimming,,hapo ndiyo unayo mistari ya matofali kwenye plasta na na rangi kama ina michirizi ya maji
8.Bati chini ya kiwango:Aisee unawekewa hata bati geji 32 na hawa watu.
*Unazijuaje
Kwa mtu ambaye siyo mjuzi wa ujenzi ni ngumu kujua...
Labda tumia ukachero wa kutumia mtu ajichanganye kupiga soga na majirani ili apate kuuliza.
*Kosa kisheria
Mi siyo mjuzi wa sheria, ila hii biashara hauwezi ita ni Utapeli, kwani bado unauziwa nyumba sema haina ubora.
Bei ikiwa ndogo, ubora wa bidhaa hupungua, hii ipo hata kwenye vifaa vya umeme,magari na hata nguo.