Poker
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 5,445
- 14,828
- Thread starter
- #181
Tuendelee brothers and sisters Good evening!
Baada ya umeme kukatika nyumba nzima, ukimya ulitawala nje na ndani. Mkenya hofu ilimtanda sana ikabidi ashuke chini mdogo mdogo katika lile giza maana aliogopa kuwasha tochi ya simu asije akaonekana location alipo. Wakati akishuka alisikia maji yanatoka huko jikoni, moyo ukazidi kwenda mbio. Ikambidi awashe tochi aende mpaka jikoni alipofika akafunga ile koki kimya kidogo kilitawala ghafla akasikia sauti ya mtoto mdogo akicheka huko sebuleni ikambidi aende kucheki na huko kunanini ile amefika tuu umeme nao ukarudi.
Akatoka nje ila hakukuta mbwa hata mmoja na zile damu zote zimefutika, aliozifuta hamjui na huyo mbwa mwingine ameenda wapi pia ikabaki sintofahamu. Ikabidi arudi mbio mbio kwanza kuicheki familia yake kama ipo salama ila cha ajabu alipofika hakumkuta hata mmoja ikabidi aanze kuwaita huku akipita vyumbani kukagua na kujua wameenda wapi. Baada ya kutafuta bila mafanikio huku simu zao zikiwepo hapo ikambidi aende control room ambako ndiko system ya camera zilipo yaani ukitaka kuangalia matukio ya hiyo nyumba inabidi uingie hicho chumba. Hivyo akajaribu kutazama na kuplay back kuangalia matukio yote ila hakuona kitu si nje wala ndani ila matukio mengine yanaonekana ila ya mbwa kuuwawa na familia kupotea hayaonekani.
Mkenya akaamua kupiga simu polisi muda huo network zimerudi kutoa taarifa na kuomba msaada polisi. Kweli baada ya kama dakika 45 walifika na pia baadhi ya watu wake wa karibu. Polisi walikagua ile nyumba yote nje na ndani huku nao pia wakijaribu kutrace chochote ambacho kinaweza patikana cha kuanzia. Ila kila walipokuwa wakitafuta jitihada zao ziligonga mwamba ndipo wakamshauri asuburi siku mbili huku wakiendelea nao kuangalia njia za utatuzi.
Baadhi ya ndugu na jamaa zake walimshauri aende kwenye maombi au alete mtu wa maombi hapo ili kama kuna nguvu za giza basi zishindwe. Ukumbuke pia mkenya aliwahi tokewa na joka. Hivyo akaona huo ni ushauri mzuri, kesho yake kweli alitambulishwa kwa mtumishi vunja vunja ambaye sifa yake kuu ni kuvunja vunja madhabahu zote za kishetani. Basi mtumishi alifika siku ya kwanza akafanya maombi akaondoka. Siku ya pili nayo vivyo hivyo, siku ya tatu mtumishi aliamua kukesha hapo ili wafanye maombi ya usiku kwani alikuwa ameshaona kuna vitu haviko sawa katika hiyo nyumba.
Usiku ulifika baada ya jua kuzama nyumba ilikuwa imepooza ukimya umetanda na huzuni huku ikisindikizwa na sauti za popo wanaopita kuranda randa huku na huko. Maombi yalifanyika sana huku mtumishi akikemea maroho yote, ghafla umeme ukakatika ikabidi mkenya ashtuke ila mtumishi hakushtuka yeye. Basi wakaendelea katikati ya maombi wakasikia mtoto analia huko nje mtumishi akamwambia twende tukakemee sasa wamejileta kwa vunja vunja, wakiwa wanatoka nje hapo kibarazani kwa juu kuna taa hizi za urembo za kuning'inia basi iliachia au kukatika ikadondoka kichwani kwa mtumishi vunja vunja na kumchoma maeneo ya utosoni. Mkenya alichanganyikiwa zaidi hivo akakimbilia getini kujaribu kutoka nje kabisa ya geti, kwa ile spidi aliyotokanayo hakulifikia geti aliteleza akajigonga kwenye kingo ya ukuta zile zimezunguka ukoka!
Je nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Based on true story!