Poker
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 5,445
- 14,828
- Thread starter
- #81
Inaendelea,,,,,, fuatana nami.
Mkenya alipokuja kuzinduka alijikuta yuko baharini mwenyewe kwenye fukwe mwenyewe. Ndipo alipoenda kuomba msaada kwenye kijiji cha wavuvi hapo jirani ambao nao walimsitiri kwa kumpatia nguo na kumuhoji kulikoni! Alijaribu kueleza mkasa wake nao wakamsihi alale mpaka pakuche ndipo wafanye utaratibu wa kurudi kwake. Basi kulipo pambazuka alirudi nyumbani ambapo alikuta tayari taarifa zake zishafika kazini na polisi. Hivo ilibidi awaeleze yaliotokea na hakuna mtu ambaye alimwamini ila wakahisi ni uchovu wa kazi hivo akapewa likizo ya mwezi mmoja arudi kwao akapumzishe fuvu lake.
Turudi sasa huku kwa nduguze na Deborah ambao wao walihisi wametengwa na familia ya mume hivyo ni kama haki yao wamenyimwa, kwahyo wakaamua shari sasa maana nao wanataka mgao au mjumuisho katika mali. Hapo ukaanza ugomvi wa mali baina ya ndugu wa mume na mke. Hivyo kutokana na ushauri wa hapa na pale kaka mkubwa wa Deborah akaamua kufunga safari mpaka Tanga wilaya mkinga katika kata ya maramba. Huko alienda kwa mtaalam mmoja ambaye waliongozana mpaka mto zigi kwaajili ya kufanya shirki. Hivo walienda na mbuzi wawili na kuku mmoja, ambapo waliwachinja na kaka wa Deborah kuoga damu ya mbuzi katika huo mto zigi.( Huo mto una mamba sana na hizo shughuli zilifanyika usiku wa manane). Baada ya hapo alitakiwa kwenda huko milima ya amani napo Tanga wanapolima sana chai kwaajili ya kujifukiza yeye na damu ya kwao.
Na upande wa pili kwa kina mume sasa wao walikuwa na mtaalam wao maeneo ya kolandoto ambaye awamu hii aliwachukua kuwapeleka simiyu wilaya ya itilima eneo moja linaitwa mwamapalala kwaajili ya kwenda kukanyagia na kuongeza zaidi moto ili wao ndio wazitawale mali. Kwahiyo ikawa kila upande una kazi ya kukanyagia ili kumtokomeza mwenzake nayeye asitokomezwe.
Kwa kipindi cha kama wiki mbili hivi ndugu upande wa Deborah walikavuta kamba watatu na huku upande wa mume alivuta kamba mmoja! Kwa hiyo ikawa kama umekaa kinyonge basi utatembea hivo familia hizo mbili wakawa maadui na viapo vingi sana baina yao kutokana na mali zilizoachwa.
Mkenya alirudi kutoka likizo akiwa na ari na nguvu mpya ya kufanya kazi, hivo alianza kazi kwa fujo kwa kufuza wafanyakazi wawili kwa kosa la uzembe. Sasa siku ya siku yeye akiwa kazini na nyumbani hakukuwa na mtu hivo vibaka waliingia ndani kujaribu kutafta rizki kwa kuiba vito vya samani ambavyo waliamini visingekosekana huko ndani. Waliingia na kuvunja dirisha kisha wakakata nondo za dirisha na kupenya ndani mmoja aliingia mwingine akabaki nje na mwingine alisimama eneo la karibu na geti kusoma raketi. Mbwa walibweka bila matumaini. Aliyekuwa ndani alianza na TV alipokuwa anaibeba ili aitoe nje aliteleza nayo na kuangukia kichwa umauti ukamfika hapo hapo na damu zikichuruzika, yule aliyekuwa nje kwasababu alisikia kishindo ikabidi aende kuchungulia akamkuta mwenzie chalii na damu zimetapakaa. Hivo akaona huu ushakuwa mkosi na kilichobaki ni kusepa. Kwaio walipokuwa ndani walivunja mlango kwa ndani na geti pia dogo walivunja komeo. Walipakiana kwenye pikipiki na kuanza mwendo ila hawakufika mbali hata mbali kutokana na mwendo kasi na wenge walivaana uso kwa uso na land cruiser, hawakuomba hata maji ya kunywa. Cruiser nayo iliharibika ila sio sana. Watu wakajongea kujaribu kutoa msaada na polisi walifika na traffic. Na mke nae wa mkenya alikuwa akirudi ndipo alipokuta hekaheka hiyo akaamua afike kwanza nyumbani, naye akakuta pako tofauti geti liko wazi, mbwa wanabweka sana aliposogea kuingia ndani akapiga yowee! Huku akikimbilia nje kabisa ya geti ikabidi watu wasogee tena huko na polisi kutaka kujua kulikoni tena huku masaki leo.
Marehemu kibaka alitolewa nje na kupakizwa kwenye defender na polisi kufanya uchunguzi wao na kuchukua sample kaza wa kaza. Na watu wakajaribu kuunganisha matukio wakajua hao walikuwa wezi na wote hakuna aliyechomoka.
Mkenya akajadiliana kwa kina sana na mke wake kwamba hapa usalama ushakuwa ni mdogo na kilichobaki ni kuhama hii nyumba na kutafta eneo jingine litakalo kuwa na usalama zaidi maana hata watoto walishaanza kuwa na hofu na uwoga.
Alifanikiwa kupata nyumba nyingine maeneo ya namanga hivyo alirudi kumtaarifu mke wake kuwa watahama mkataba utakapokuwa unaisha. Ikiwa imesalia wiki moja, usiku mkenya alitoka nje baada kusikia mbwa wanabweka sana akahisi wamevamiwa tena. Alizunguka ila alikuta mbwa wanabweka ila hakuna kitu. Akaamua kurudi ndani tena bado akasikia wanabweka ila ghafla kimya kikatawala alitoka tena wakati huu akiwa na tahadhari kubwa, alizunguka ila hakuwaona mbwa alipokuwa akirudi mlango mkubwa wakutokea nje alimkuta mbwa mmoja amekufa na damu zinachurika tuu. Akatoa pistol yake ndogo na kurudi ndani kufunga mlango, aliiamsha familia yake na kuwaweka alert kuwa kuna hatari ivo wakusanyike sehemu moja wakati anafanya mpango wa kupiga simu polisi. Akiwa kwenye harakati za kupiga simu network haikamati ikabidi amwombe mke wake simu na yenyewe pia network haikamati! Hofu iliwatanda wote na presha ikawa juu yao, yule mbwa mmoja ghafla akaanza kubweka tena mwenzake ameshauwawa, ikambidi mkenya achungulie dirishani maana ndani ni giza na nje kuna mwanga hivo akiwa katika harakati za kuzungukia madirisha kuchungulia na kuyafunga ghafla bin vuu! Umeme ukakatika nyumba nzima,,,,,,,
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Iko based on true story kabisa ilio tokea hapa hapa TZ ila locations na majina sio halisia.