Nyumba ya mchungaji Mtikila yauzwa na Bank

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
6,559
Reaction score
12,518
Nyumba ya mjane wa marehemu Mchungaji Christopher Mtikila, Bi. Georgia Christopher Mtikila, iliyopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, imekumbwa na taharuki baada ya watu wanaodaiwa kufika nyumbani kwake kutoa baadhi ya mali zake nje na kisha kubadilisha vitasa vya milango wakidai kuwa nyumba hiyo imeuzwa na benki.

Akizungumza na Global TV, Bi. Georgia amesema kuwa mwaka 2018 aliwahi kumdhamini kijana aitwaye Ramadhani Seif kupata mkopo wa benki wa shilingi milioni 250. Kwa mujibu wake, kijana huyo aliletwa kwake na rafiki wa marehemu mchungaji huyo kwa ajili ya kupata udhamini huo.

Bi. Georgia amesema kuwa Ramadhani Seif aliwahi kuanza kurejesha mkopo huo, lakini baadaye alishindwa kuendelea kufanya hivyo baada ya biashara yake kudorora na hatimaye kufeli.

Hata hivyo, hali hiyo imeibua sintofahamu kufuatia hatua ya watu hao kufika nyumbani kwake na kudai kuwa nyumba hiyo imeuzwa na benki kutokana na deni la mkopo huo.

Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa Mtaa husika, Nelson Saidi, zinaendelea ili aweze kuzungumzia sakata hilo na kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu tukio hilo.

Chanzo : GlobalTv
 
Marafiki ni tatizo sana kwenye jamii zetu Afrika.
 
Hapa ndio watanzania tunakuwaga na unafiki wa sgr.

Yeye mwenyewe kakubali kuwa aliweka nyumba kama dhamana ya mkopo na kakubali kuwa kijana kashindwa kulipa mkopo tangu 2018 sasa mnataka bank ifanye nini?

Eti mnasema imeleta taharuki! Taharuki ya nini na nyumba iliwekwa dhamana kwa mkopo ulio default?

Tena tangu 2018!!

Tuache unafiki, nyumba iuzwe bank ipate haki yake
 
Daah kwa biashara zilivyo unaenda kuchukua Tsh 250m aisee kwa dhamana ya nyumba labda angekua na tender ya kusambaza mafuta mikoani au DRC ndio angetoboa kwa kuwa na Scania 4 kutoka kwa kaburu..
Kwa miaka hiyo kodi ya Truck ilikua haijapandishwa tofauti na ilivyo sasa Majambazi wanataka wafanye biashara ya Logistic wao tu huku magari wakipitisha bila kulipa kodi kubwa.
 
Mtu akifa mkopo hulipwa na bima wala hawaji kuchukua mali!

Ndio kazi ya bima!
Isipokua kama upo hai na umeshindwa kulipa ndio wanakuja kuuza maana hayo yanakua makusudi
Umesoma ukaelewa? Mtkila kafariki miaka mingi iliyopita. Anasema mkopo umechukuliwa 2018, tena kupitia kwa kijana aliyemdhamini lakini baadae akashindwa kulipa.
 
Huyu mama mjinga hapo watoto wakazuie kwa sababu hawakushirikishwa, huo ni utetezi si ajabu walipewa kitu kidogo.

Watoto wanazuia kwani nyumba ni yao?
Hati imeandikwa jina la nani?

Huyo Mama ndiye Mmiliki wa hiyo nyumba. Ametoa kwa hiyari nyunba yake uwe rehani kwa huo Mkopo.
Sasa watoto wanahusikaje?

Rafiki wa mumewe? Kijana akakopa😀😆
 
Bi. Georgia amesema kuwa mwaka 2018 aliwahi kumdhamini kijana aitwaye Ramadhani Seif kupata mkopo wa benki wa shilingi milioni 250.
Bi. Georgia amesema kuwa Ramadhani Seif aliwahi kuanza kurejesha mkopo huo, lakini baadaye alishindwa kuendelea kufanya hivyo baada ya biashara yake kudorora na hatimaye kufeli.
Duh,
Huyo mama alifanya maamuzi ya hovyo, ukute yalikuwa maamuzi ya hisia badala ya akili
 
Huyo mama ni juha
Mtikila huko aliko anasikitika sana
Walokole ndivyo walivyo.. Ukute huyo kijana aliletwa na Baba Mchungaji.

Hata hivyo sijaelewa.. Yeye alidhamiini Mtu au aliomba Mkopo kwa dhamana ya nyumba? Yaani kadhamini mtu naye akajidhamini kwa nyumba?

Nilijua anayekopa ndo anatakiwa kupeleka mali isiyo hamishika.. Wengine mnakuwa wanadhamini kwamba mnamjua na hiyo mali ni yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…