Tetesi: Nyumba ya mjane wa Balozi John Rupia Katibu Mkuu Kiongozi (mstaafu) yadaiwa kupigwa mnada

Nimekupata Paskali ,nimeona tu kwamba wana undugu naye na kuifadhili TANU....ila kwenye kupigania uhuru sijaona labda anaweza kutuambia kama alikuwa na mchango kwenye kupiania uhuru.
Duh, hivi wewe ni Mtanzania mwenzetu kweli unauliza kama Mzee John Rupia ana mchango kwenye kupigania uhuru!. Shukuru sana immigration yetu wamelala sana, vinginevyo hii ni nyama ya bure bure, nje nje!.
P
 
Nyumba kuwa matrimonial home sio kuwa haikubaliki kukopea pasipo sign ya spouses wote, Mahakama ya Rufani iliweka sawa hili suala katika kesi ya SAUDA MLIMAKIFI kuwa kama jina linalosoma katika hati ni la spouse mmoja basi inatosha kabisa kuthibitisha kuwa ni yake, huyo spouse mwingine kama anaona ana interest na hiyo nyumba basi akafanue usajili hata kwa CAVEAT ili jina lake liingie kwenye rekodi na hivyo kufanya takwa la yeye kusaini mkopo liwe la lazima. Ila kama hajasaini hati, hata kama nyumba ni matrimonial home inaweza kukopewa kwa mwenye jina kwenye hati kusaini yeye pekee.

Izingatiwe, matrimonial home ni nyumba wanayoishi wanandoa na iliyopatikana kwa juhudi za wanandoa wote wawili, kama hawaishi hapo ila wameipata pamoja kwa ushirikiano basi inaitwa matrimonial property.
 
Nguli huyo mohamed said.
Maelezo safi; kwenye hiyo story nimefurahi kuwataja watu niliyowajua Lameck Nicodem Ubwe na wadogo zake jacob na saul
 
Izingatiwe, matrimonial home ni nyumba wanayoishi wanandoa na iliyopatikana kwa juhudi za wanandoa wote wawili, kama hawaishi hapo ila wameipata pamoja kwa ushirikiano basi inaitwa matrimonial property.
Mkuu sajo , asante umenielimisha kitu kizuri kuhusu nyumba ambayo ni matrimonial home na nyumba ambayo ni matrimonial property, kwasababu Balozi Rupia alikuwa na lots of family properties za urithi ambazo sio matrimonial properties
P
 
Nyuma ya wazo yenyewe wana eneo kubwa sana kulikuwaga na crusher wanapasua kokote,muda sana hawafanyi kitu..
Mpaka hapo inaonesha ni jinsi gani watoto, wajukuu walivyo wanashindwa simamia miradi
Wao ni kula bata,safari na shopping za ulaya nyingiii

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…