Kwahiyo?Huyu mama ni msharika mwenzangu pale St Albans
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwahiyo?Huyu mama ni msharika mwenzangu pale St Albans
Duh, hivi wewe ni Mtanzania mwenzetu kweli unauliza kama Mzee John Rupia ana mchango kwenye kupigania uhuru!. Shukuru sana immigration yetu wamelala sana, vinginevyo hii ni nyama ya bure bure, nje nje!.Nimekupata Paskali ,nimeona tu kwamba wana undugu naye na kuifadhili TANU....ila kwenye kupigania uhuru sijaona labda anaweza kutuambia kama alikuwa na mchango kwenye kupiania uhuru.
Nyumba kuwa matrimonial home sio kuwa haikubaliki kukopea pasipo sign ya spouses wote, Mahakama ya Rufani iliweka sawa hili suala katika kesi ya SAUDA MLIMAKIFI kuwa kama jina linalosoma katika hati ni la spouse mmoja basi inatosha kabisa kuthibitisha kuwa ni yake, huyo spouse mwingine kama anaona ana interest na hiyo nyumba basi akafanue usajili hata kwa CAVEAT ili jina lake liingie kwenye rekodi na hivyo kufanya takwa la yeye kusaini mkopo liwe la lazima. Ila kama hajasaini hati, hata kama nyumba ni matrimonial home inaweza kukopewa kwa mwenye jina kwenye hati kusaini yeye pekee.Mkuu peno hasegawa, asante kwa taarifa hii.
Nyumba yoyote inapopigwa mnada maana yake ni imetumika kama collateral for loan.
Kama nyumba hiyo ni matrimonial home, haikubaliki as a collateral mpaka both spouses wasaini.
Mke kama ulisaini nyumba itumike as collateral, mume akachukulia mkopo, baadae mume akafa bila kuulipa huo mkopo, kifo cha mume hakifuti lile deni la ule mkopo, hivyo mkopo lazima ulipwe!. Ukishindwa kulipa, ujane sio an excuse kuizuia bank to recover its debts.
Huu ni mfano mzuri wa kuwafundisha Watanzania kuweka bima, kuna mpaka bima za mikopo, ukifa kabla hujamaliza kulipa mkopo, bima ina take over na kukulipia!.
Rupia ni among the top ten giant families zenye lots of properties jijini Dar es Salaam!. Yale maghorofa yote matatu pale Uhuru Roundabout ni ya baba yao Mzee John Rupia, ambapo wakati wa utaifishaji hayo hayakuguswa!.
Hivyo hilo la hii nyumba ni dogo tuu!.
Pole Mama Anna, hili ni dogo tuu kama upepo na litapita tuu!.
P
Nguli huyo mohamed said.KIFO CHA BALOZI PAUL RUPIA: DAR ES SALAAM TUMEFIWA
Sidhani kama kuna mtu ana ujasiri wa kunyanyua kalamu yake pale Abdallah Tambaza atakapoandika historia yoyote inayuhusu Dar es Salaam iwe matukio au iwe taazia.
Naitazama taazia ya Balozi Paul Rupia baada ya kumaliza kuisoma na kuna kitu kinachogonga kichwani kwangu kama vile kuniuliza, ''Hivi kweli huna lolote la kusema kuhusu Balozi Paul Rupia?''
Najijibu mwenyewe, ''Vipi nitakosa la kusema kuhusu Balozi Rupia ilhali nimemfahamu kwa miaka mingi na kwa mbali ni jamaa yangu kwa nasaba ingawa ya mbali kwangu binafsi?''
Haya nitakayosema hapa huenda yakawashtua na kuwashangaza wengi.
Ishatokea hivi mara nyingi.
Udugu wetu na ukoo wa Rupia unatoka mbali sana kutoka kwa bibi yetu mkuu Bi Christina mama ya bibi yetu Bi. Deborah Mgone (1890 - 1995).
Bibi zetu hawa ndiyo waliotuunganisha na ukoo wa Rupia.
Sisi leo ni kizazi cha nne kutoka kwa bibi yetu mkuu Bi. Christina.
Hapa unazungumzia historia inakaribia miaka 200.
Kama walivyo akina Rupia kuwa wana nyumba Misheni Kota nasi pia tuna nyumba mbili Misheni Kota hadi leo.
Nyumba nyingine tatu ziko Mtaa wa Swahili moja, Sikukuu zilikuwa mbili sasa imebaki moja.
Moja bibi aliuza.
Hii ilikuwa jirani sana na Saigon Club.
Nyumba hizi tumezaliwa tumezikuta.
Hatujui lini zilijengwa.
Naamini hizi nyumba sasa zina umri zaidi ya miaka 100.
Nyumba hizi zinatukumbusha utoto wetu na kututafsiria mengi katika maisha yetu.
Bi. Christina na Bi. Deborah niliowataja hapo juu hawa wote mimi nimewaona kwa macho yangu na wameondoka duniani mimi nina fahamu zangu kamili.
Na katika dada zetu alikuwapo Christiana kapewa jina la bibi yetu mkuu maarufu tukimwita ''K'' (apumzike kwa amani).
''K'' alikuwa mkubwa kidogo kwangu na alinipokea St. Joseph's Convent School 1967 na yeye alipokewa hapo na kaka yetu Charles Mgone 1965 au 1966.
Ndani ya historia hii vipi nikose la kusema kuhusu Balozi Paul Rupia na ukoo wa Rupia wenyewe na historia ya wazee wetu waliokuwapo wakati sisi tunazaliwa na kaka zetu tuliowakuta mfano wa marehemu Albano, Balozi Rupia na Steven maarufu kwa jina la Mpuya?
Hawa walikuwa watu maarufu bila ya hata kujikwaza.
Nimehudhuria shughuli nyingi na Albano akiwepo lakini huwezi kusikia sauti yake.
Yeye siku zote alikuwa mtu wa kusikiliza.
Mzee Albano alikuwa mtu wa maneno machache mno.
Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nilikutana na barua iliyoandikwa na Makata Mwinyimtwana anamwandikia Ally Sykes kuhusu mwanae Makata ambae alikuwa anakwenda kusoma Liberia pamoja na Paul Rupia kwa scholarship ya TANU.
Barua hii nasikitika sana leo kuwa sikuitia maanani asilani.
Nimeisoma nikapita.
Ninachokumbuka ni kuwa Mzee Makata Mwinyimtwana alikuwa anatafuta ushauri kutoka kwa Ally Sykes kuhusu hali ya baadae ya vijana hawa waliokuwa wanakwenda nje kupata elimu ya juu.
Katika msafara huu wa kwenda Liberia alikuwako Ngombale Mwiru.
Huyu Makata Mwinyimtwana kama alivyokuwa John Rupia alikuwa Mwafrika tajiri sana Tanga.
Inafahamika na wengi kuwa Balozi Rupia hakuwa anapenda kueleza si historia yake wala ya baba yake.
Naamini kabisa kama angenyanyua kalamu kuandika kumbukumbu zake hakuna wasiwasi kuwa historia ya baba yake ingefahamika na mengi ambayo leo yanababaisha watu yangekuwa hadhir.
Naikumbuka Misheni Kota ya 1960s na kilichokuwa kinanipeleka ni kuwa hii ilikuwa miaka ya ''Soul Music'' - James Brown, Aretha Franklin, Ottis Redding, Wilson Pickett, Sam and Dave halikadhalika Erick Burdon and The Animals, Mick Jagger and The Rolling Stones, The Beatles nk.
Muziki wa Wamarekani Weusi na Misheni Kota kulikuwa na vijana wapigaji muziki huu katika bendi maarufu za vijana Sparks na The Rifters - akina Sauti Plantan, Lameck Nicodemus Ubwe na wadogo zake Jacob na Esau.
Nikishinda Misheni Kota siku za likizo - ''jam sessions.''
Nikifika hadi nyumbani kwa Mzee Rupia kwa hili au lile na naikumbuka sana ile mikungu iliyokuwa pale nje.
Lakini sikuwa naijua historia ya nyumba ile kuwa ndipo mkutano wa kuunda African Association ulipofanyika mwaka wa 1929 na wakati ule nyumba ile ilikuwa ya Cecil Matola John Rupia akaja kuinunua baadae.
Haya nilikuja kuyajua baada ya kumsoma Daisy Sykes katika kitabu alichohariri John Iliffe.
Nilipokuwa mazikoni tena niko na Abdallah Tambaza nimemuona Ayoub Sykes na dada zake Guru na Miski, Said Mpango na dada yetu Bi. Baya kutoka Msasani wamekuja mazikoni wamebaba maua wamekuja kumzika kaka yao mkubwa Balozi Rupia.
Babu yao Kleist Sykes alikuwa rafiki mkubwa wa John Rupia ndani na nje ya siasa za African Association na barza yao kubwa ilikuwa nyumbani kwa Keist Mtaa wa Stanley na Sikukuu jirani na nyumba ya bibi yangu Bi. Deborah na jirani ya nyumba ya Mzee Maleta na Mzee Kubbe.
Sasa miaka 73 imepita baada ya kifo cha Kleist na kuvunjika kwa ile barza.
Wajukuu ni sisi na tumeihifadhi historia hii ndani ya vifua vyetu.
Paul Rupia kwangu alikuwa ni kaka mkubwa wala sina maingiliano yoyote na yeye.
Wala sikuwa najua kuwa kuna ujamaa baina yetu.
Haya nilikuja kuyafahamu baadae sana.
Mimi na wenzangu Paul Rupia alikuwa ni kaka tu kama walivyokuwa kaka zetu wengine wa Misheni Kota kama Kurwa na Doto Plantan, Malombe, Denis Nicodemus Ubwe kwa kuwataja wachache, wakati ule anasoma Chuo Kikuu Cha Nairobi.
Dar es Salaam tumefiwa.
Balozi Paul Rupia ni sehemu ya historia ya Dar es Salaam.
Tumefiwa na mtu ambae kaona yote kwa macho yake na kaishi maisha ya nyakati zile na kwa hakika alikuwa hazina kwetu lau kama alikuwa kimya katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ingawa baba yake alikuwa mmoja kati ya waasisi wa TANU na wafadhili wakubwa Balozi hakupenda kueleza haya.
Balozi Rupia yeye kwa ile tabia na hulka yake ya unyofu hakupenda kueleza historia ya Rupia katika kupigania uhuru wa Tanganyika na kuwa baba yake alikuwa mmoja wa nguzo kuu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kaka yetu Balozi Rupia huyu hakutukataza kuandika historia hii yetu kwa faida ya vizazi vijazo ingawa yeye mwenyewe maisha yake yote alikuwa kimya.
Balozi Paul Rupia katuachia funzo.
Kaka yetu Paul Rupia ni hadithi nzuri ya kuhadithiwa, chembelecho Rais Ali Hassan Mwinyi.
PICHA:
Picha hizo hapo chini nimempiga Balozi Paul Rupia akiwa na mkewe Bi Rose Desta na kaka yangu Charles Mgone akiwa na mkewe Bi. Joyce Bakuname siku ya harusi ya mwanetu Harold.
Picha hiyo ya chini wa kwanza kulia ni shangazi yetu Bi. Flora Mgone.
![]()
![]()
Mkuu sajo , asante umenielimisha kitu kizuri kuhusu nyumba ambayo ni matrimonial home na nyumba ambayo ni matrimonial property, kwasababu Balozi Rupia alikuwa na lots of family properties za urithi ambazo sio matrimonial propertiesIzingatiwe, matrimonial home ni nyumba wanayoishi wanandoa na iliyopatikana kwa juhudi za wanandoa wote wawili, kama hawaishi hapo ila wameipata pamoja kwa ushirikiano basi inaitwa matrimonial property.
Endeleeni kumuombea msharika mwenzenu anapitia kipindi kigumu kisaikolojia.Huyu mama ni msharika mwenzangu pale St Albans
Tutazidi kumuombeaEndeleeni kumuombea msharika mwenzenu anapitia kipindi kigumu kisaikolojia.
Sijui walikopa fedha za kifanyia nini
Nyuma ya wazo yenyewe wana eneo kubwa sana kulikuwaga na crusher wanapasua kokote,muda sana hawafanyi kitu..Most 1st class families, wame invest kwenye real estate, shares, bonds na stocks, hivyo mzigo upo wa kutosha tuu, ndio maana watu tuko surprised what's happening hadi hii property iuzwe kwa mnada!. Hata ingekuwa inadaiwa, ni Mjane anapiga tuu hodi kwa The King Maker, mzigo unawekwa mezani!. I do suspect this is a deal!.
Kwenye big business world sometimes one has to cut your coat to spite your face!. Jicho likikuponza, unaliondoa na kubaki na jicho moja ili kuuokoa mwili, kuliko kuupoteza mwili wote mzima mzima mazima!
I smell something fishy about this!. Kwa watu tunaomjua Balozi Rupia, ana bonge la jumba la kufa mtu Masaki, kwanini aliendelea kuishi hapo kwenye hicho kijumba?, it must be ni for a reason!. Ila pia there must be something unusual kuhusu hiyo nyumba, kwasababu the location ni prime, ukubwa wa plot ni low density, angalia nyumba nyingine around halafu linganisha!. That was an investment potential tena a huge investment!, why it was never developed?!. Hapo kuna something behind sio bure!. Isije ikawa ni ... house!, hiyo ... naomba nisiiseme maana nyumba iko sokoni mnadani, kuna siri zikitoka tuu!, haizuki!, hivyo tusiharibu biashara za watu!.
P
Matumizi tu [emoji1]Endeleeni kumuombea msharika mwenzenu anapitia kipindi kigumu kisaikolojia.
Sijui walikopa fedha za kifanyia nini
Yap alipe deni la watukama wanadaiwa why not? hakuna namna., dawa ya deni ni kulipa tu uwe mjane ama mgane.
Walipe hakuna namnaMkuu lakini si walikopa na wameshindwa kirejesha?. Usikute hapo kijana ndo kakopa alafu mjane ni mdhamini.