Mkuu pole sanaa, ila kwa uzoefu tu, ni kwamba wewe unapaswa kuwasiliana na NMB ili mkalijadili ilo swala kwakua lina jadilika na uwaambie kuanzia sasa wewe ndio unachukua jukumu la kuulipa mkopo huo, waambie wewe una interest na nyumba hio kwakua ni yako, na hapa mtaelewana, na hii njia imewasaidia wengi tu, wengine mpaka wanaongezewaga muda.
Ila endapo jamaa watakua wako serius wamedhamilia kuuza basi utakua hauna budi kwenda kufungua kesi ya msingi dhidi ya madai tajwa na kuweka zuio la muda mahakamani chini ya hati ya dharula kuzuia kuuzwa kwa nyumba hio ukiwa na sababu kuu tatu ambazo ni;
1. Hasara utakayoipata baada ya kuuzwa hio nyumba ni hailipiki kwa namna moja au nyingine.
2. Una sababu za msingi sanaa za kuzuia nyumba hio kuuzwa kwakua ikiondoka itasababisha maafa makubwa.
3. Tayari umefungua kesi ya msingi dhidi ya swala ilo ivyo unaomba kuzuia nyumba hio ambayo ni sehemu ya kesi uliyoifungua isiuzwe.
Mengine watafte wanasheria walio karibu yako wakusaidie kama utaona mlolongo unakua mrefu zaidi.