Nyumba za kuishi zinazojengwa na wasomi wa siku hizi zinafikirisha

Nyumba za kuishi zinazojengwa na wasomi wa siku hizi zinafikirisha

Kijogoodi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
1,362
Reaction score
2,373
Habari

Nimefanya utafiti wa nyumba za kuishi zinazojengwa na vijana wasomi kuanzia degree moja na kuendelea kwa kweli zinafikirisha!

Msomi mzima na kazi yake anakutambia amejenga lakini ukimtembelea kwenda kuona nyumba aliyojenga unabaki kujiuliza hii ni nyumba ya mtu aliyetumia miaka zaidi ya kumi darasani kweli? Ramani haieleweki na jumla ya vyumba alivyojenga ni sebule,chumba chake na chumba cha watoto baasi!

Ni uchoyo ili wasije wageni au ni ukosefu wa hela?

Mbona sisi wasomi wa zamani tulikuwa tunajenga mabangaloo ya kufa mtu?

Wasomi wa siku hizi jirekebisheni nyumba zenu ni sawa tu na ya mkulima wa pamba ambaye anauza na kupata hela mara moja kwa mwaka.

IMG-20190705-WA0019.jpg
 
Fisad mkubwa wewe tunakujua tangu siku nying imeibia ofis ya serikal ukajenga utopolo wako sasa unajisifu hapa

Je unataka na sisi vijana tuibe kama wewe?
 
Habari

Nimefanya utafiti wa nyumba za kuishi zinazojengwa na vijana wasomi kuanzia degree moja na kuendelea kwa kweli zinafikirisha!
Ramani haieleweki na jumla ya vyumba alivyojenga ni sebule,chumba chake na chumba cha watoto baasi!
Ni uchoyo ili wasije wageni au ni ukosefu wa hela?

Mbona sisi wasomi wa zamani tulikuwa tunajenga mabangaloo ya kufa mtu?
View attachment 1850404

Nilipoona title ya uzi wako, na nilipofungua huu uzi na kukutana na picha nikashwishika kusoma maelezo ya uzi nikiamini kuna maelezo ya kihandisi yameandikwa yakichagizwa na picha (ukichukulia huo ukuta unaonekana una kasoro ikiwemo kukosa nguzo kwenye kona)...

Lakini imekuwa kinyume na matarajio yangu, kumbe ni 'uzi mipasho' na yaonesha ni kama mleta mada amepatwa na stress toka kwa watu anaowazungumzia...
 
Wapi qasomi wa degree 3 hata huo msingi hawana tunagombana nao huku kwenye kuuza maji barabarani, afu we unasema habari za usoni na maisha halisi.
 
Kwa hiyo nanusomi wako mzuri wa zamani ndo uka come up na huu uzi? Kweli upo miaka ya 47. Pole yako, nawaonea huruma wajukuu zako.
 
Kua msomi haimaanishi utakua na maisha mazuri bali usomi(elimu) ni njia mojawapo Kati ya njia nyng za kua na maendeleo....sasa mtoa mada unashndwa kutofautisha Mambo halaf una mtazamo wa kipumbavu Sana
 
Siku hiz tunafamilia kubwa mshahara mdogo, kidume unamademu watano nyumban una mke na watoto wa wili bado wazazi kidume me ndio tegemeo Bangalo litoke wap ata kupata hivyo viwili tu vyumba mungu anisahidie
 
Nyumba za zamani na za sasa zipi nzur?
 
We kaa kwako mkuuu kelele nyingi za nini!!!? 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom