Nyumba za kuishi zinazojengwa na wasomi wa siku hizi zinafikirisha

Nyumba za kuishi zinazojengwa na wasomi wa siku hizi zinafikirisha

Kumbuka anajenga kwa mkopo, mkono unajikuna mahali unapofika . Nyakati za nyuma gharama za kujenga zilikuwa poa kidogo
 
[emoji16][emoji16][emoji16] ngoja nicheke tu ...ukute unajiongelea we mwenyewe
 
Habari

Nimefanya utafiti wa nyumba za kuishi zinazojengwa na vijana wasomi kuanzia degree moja na kuendelea kwa kweli zinafikirisha!
Msomi mzima na kazi yake anakutambia amejenga lakini ukimtembelea kwenda kuona nyumba aliyojenga unabaki kujiuliza hii ni nyumba ya mtu aliyetumia miaka zaidi ya kumi darasani kweli? Ramani haieleweki na jumla ya vyumba alivyojenga ni sebule,chumba chake na chumba cha watoto baasi!
Ni uchoyo ili wasije wageni au ni ukosefu wa hela?

Mbona sisi wasomi wa zamani tulikuwa tunajenga mabangaloo ya kufa mtu?

Wasomi wa siku hizi jirekebisheni nyumba zenu ni sawa tu na ya mkulima wa pamba ambaye anauza na kupata hela mara moja kwa mwaka.View attachment 1850404
umeamka kwenda kukojoa ndio ukaandika huu uzi.
 
Kuna usemi unasema Kichaa huwa anaona wenye akili timamu ndo vichaa. hapa mtoa mada hujui maana ya kutumia pesa ulizonazo vizuri. pia usisahau mafanikio sio nyumba, wapo matajiri wakubwa duniani wanakaa kweny nyumba za kupanga au mkopo ili waweze kutumia pesa zao vizuri kuanzisha na kukuza biashara zinazozalisha, na sio kwenda kuzika pesa kweny liability isiyokupa hata sent 5 kwa mwaka. Jifunze kidogo wa Bilionaire Warren utajua kwa nini hao uliowaita wasomi wamekupita mbali kifikra.
 
Warren hana nyumba?
Anakaa kwenye nyumba ya nani?
Hiyo nyumba aliyopanga si analipishwa kodi?
 
Sasa unataka watu wajenge nyumba kubwa nani analala huko? Jenga nyumba ya saizi yako mzee.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Nakubaliana na wewe.

Hayo majumba makubwa ya kizamani yana faida gani? Siku hizi watoto wakimaliza shule na kuanza kazi hawataki kukaa nyumba ya familia wanakwenda kutafuta maisha kivyao. Wewe umebaki na bangaloo lako la kufa mtu (kwa maneno ya mleta hoja), munatumia vyumba viwili cha kwenu (Mr and Mrs) na mfanyakazi.

Kwa faida gani maintenance costs ziwe kubwa bila sababu? Ukistaafu kapension chenyewe kiduchu unashindwa kulihudumia, matokeo yake umebaki na gofu.

Haya ndiyo yanayowatokea wastaafu wengi wa kipindi kile.

Leo vijana wameamka wamejifunza kutoka kwa wazee wao.
 
Back
Top Bottom