Nyumba za kupanga ni vijiji ndani ya miji


Zinaa ni kubwa Sana za kuzungukana wapangaji sababu wanashare vingi hivo upelekea ushawishi.
 
Uswazi tunazaa sana..kipindi hiki Cha likizo yaani utafikiri tuko kwenye ile kambi maarufu ya wakimbizi kule Kenya..na ndio maana hata shule wanaingia kwa shifti..just imagine kuna darasa A mpaka G...yaani ni balaa.
 
Uswazi tunazaa sana..kipindi hiki Cha likizo yaani utafikiri tuko kwenye ile kambi maarufu ya wakimbizi kule Kenya..na ndio maana hata shule wanaingia kwa shifti..just imagine kuna darasa A mpaka G...yaani ni balaa.
Huku kwetu mtoto akijua lugha ya pili ni Kizaramo au Kindengeleko. Mtoto akisema good morning anaitwa mtoto wa Kizungu.
 
Nyumba za kupanga ilikua ni chalenge sana kwa sisi mabachela wa enzi hizo. Ukiingiza demu ndani kwako ujue ukimuamkia mama mwenye nyumba hawezi kuitikia. Na ukirogwa uingie kwenye kumi na nane zake ndio utamjua mzaramo anaweza kuua kwa kusuta. Halafu ukiingiza demu ndani kwako wanawake wote wanahamia uwani karibu na choo ili mtoto wa watu apewe vijembe mara akiingia chooni. Waswahili. I hate you
 
Hata ukipikia gesi ndani ukiwa unaosha vyombo nje atatumwa mtoto aje aangalie ulipika nini.
 
Kuna kipindi napanga. Basi kuna mwanamke mmoja alikua hajaolewa, alikua anafanya BIMA. Basi alikua anatembelewa na wanaume kila mara. Kumbe kile kitendo cha kutembelewa na njemba kilikua kinamuudhi baba mwenye nyumba. Choo kilikua ni kama kimejaa na hakina roof yaani ukiingia unaona mizigo yoye fresh. Sasa baba mwenye nyumba kuingia toilet akakuta kuna $@#ndom zilizotumika zinaelea juu. Alimwita mama wa BIMA na kumpasha kwamba yeye mama bima ndio mtumiaji wa $$ndom pekee kwa hivyo akaondoe €ondom zake chooni. Aisee yule dada nilimhurumia na alidhalilika.
 
Huyo jamaa Ni mwoga tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyumba za kupanga ni kero, niliwahi kuishi moja ya wapangaji wengi ubungo.. ilikuwa mimi natoka asubuhi sana so ilikuwa lazima mi ndo niamke wa kwanza kuoga. Sasa lile bafu ilikuwa ni choo hapo hapo, aisee ilikuwa tabu sana ile asubuhi nlikuwa nakutana na harufu moja kali sana, ilikuwa lazima ni mwage maji kama ndoo moja ndo nioge. Nliteseka sana, tangu nihame hapo sijawahi tena kushare bafu na choo.. never
 
Haya ndiyo maisha halisi ya 1/2 ya wana Dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…