Nyumba za kupanga ni vijiji ndani ya miji

Unaoga saa sita usiku au 11 asubuhi u
 
Hivi siku hizi zile nyumba za kupanga za six rooms corridor katikati, jiko na bafu uani halafu uani kuna kijigeti bado zipo?
Mwenye nyumba chumba chake ni cha mbele kutizama barabara halafu nje kuna kochi la zege bado zipo??
 
Siku hizi mbona kuku wamekua wakawaiida hadi kudharaulika. Enzi hizo mkiwa nyumba ya kupanga mtu anaekula kuku mara kwa mara alikua mfanyakazi wa RTC au ugawaji. Vinginevyo hawa wengine kuku hadi idd el fitr.
 
@Sky Eclat

Ni Breach of Privacy. Not "Breech".

No hate though, just correction.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu Sky Eclat alisoma kipindi kile shule yoyote english medium inaitwa International au Academy. Iweje leo akosee spelling?😂😂😂😂
Eclat alisoma st Mary's ila kampas sina uhakika nayo. Kulikua na Mbezi kampas. Tabata na Mbagala.
 
[emoji23][emoji23]

Madame Sky Eclat yupo smart sema vidole vilicheza.

Ila campus itakuwa mbagala maana uswahili anaujua nje ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hatujafunga huu mjadala wa nyumba za kupanga. Kuna jamaa alimtembelea mpangaji mwenzetu Dar akitokea mikoani. Mama mwenye nyumba hakupendezewa na ujio wa yule mshamba. Kuna mtoto katumia choo bila ku flush. Mama mwenyenyumba kalianzisha akijua yule mshamba anasikia na watu wote. Jamani kuna mtu hajui kutumia choo kwenye hii nyumba, kina mama wote wambea na wasio wambea wakaanza kumsapoti mwenye nyumba ikawa ndio tukio la siku. Mtu huyo atakua ni mgeni humu maana haijawahi kutokea. Aisee yule mshamba alikua mdogo kama piriton. Kwenda chooni alikua anakwenda usiku kwa usiku na muda wote yuko chumbani. Kumbuka enzi hizo hakuna TV Ila joto lilikuwepo
 
Hivi wanawake wa Kiswahili mna nini lakini. Ukimpeleka gesti mnafanya kimya kimya. Sasa hebu afanywe kwenye nyumba ya kupanga isiyo na ceiling board. Si kilio hicho utadhani ameingizwa jiwe. Huku kitanda nacho ni swikwq swichwiq $#@€
 
Hahahahaha dah bro ulikula adhabu sana ilikua wap hiyo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar ukisikia chumba ni chini ya laki unusu usihangaike kwenda hata kukiona
 

Hadi leo hujawahi tena kushea?
 

Baada ya hapo (kupigwa laptop) ukahama?
 
Hivi siku hizi zile nyumba za kupanga za six rooms corridor katikati, jiko na bafu uani halafu uani kuna kijigeti bado zipo?
Mwenye nyumba chumba chake ni cha mbele kutizama barabara halafu nje kuna kochi la zege bado zipo??

Mwananyamala zimejaa tele!
 
Sky hili la kusema 'mababa wenye nyumba' pia wapewe vyeo vya 'ukitongoji' au 'watendaji wa mtaa', kwa kuwa ni wamiliki wa kaya nyingi ndani ya 'mapango' yao, siyo sahihi.

Kumiliki nyumba siyo busara ya kuongoza jamii, hauonagi madhaifu ya wenye nyumba ya kulazimisha kupewa mboga?

Labda ungelisema kuwa pango likizidi wakaazi kadhaa kukidhi akidi za uchaguzi,basi chaguzi zitembee pangoni mumo kwa mumo kidemokrasia ili hata kama ni mpangaji kura ikimwangukia awe kiongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…