Nyumba za kupanga za kuchangia choo na bafu ni maisha duni sana.

Nyumba za kupanga za kuchangia choo na bafu ni maisha duni sana.

Kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga ambapo mnachangia choo na bafu na wapangaji wengine basi bado unaishi katika maisha duni sana, bado una safari ndefu ya kuyafikia maisha ya hadhi anayostahili binadamu.
ni kweli
 
Wakati nasoma Chuo, nilipata room kwa tabu sana na bei kubwa it was 50k per month. Sasa room ni single, choo kipo na bafu hapo hapo yaan unakata gogo unaoga kabisa.

Choo hakina mlango wala bati juu ni pako wazi, mpk ufike chooni utembee hatua kama 15 hivi.. upite corridor lenye vyumba vinavyoangaliana.. sometimes Mama mwenye nyumba na wapangaji wengine unawakuta wametandaza miguu inabidi uwaruke uende kuoga.

Ndani nina ndoo mbili, maji kuchota ni mtaa wa nyuma..

Ni Mwananyamala kwa Kopa hiyo.. ndio watu tunaanza life, alafu Pisi zilikuwa zinakuja na kukubaliana na hali hivyo hivyo😂.

Now aisee mambo yamechange bhana, ili kuingia kwangu lazima upande Elevator 😂..

Ni swala la muda, kila kitu kina muda wake na hakuna kitu kizuri kama kuanzia chini, hali zote za Maisha unazijua..
 
Back
Top Bottom