BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Hapa ni Jumba Namba Nne - Michenzani usawa wa geti na RahaLeo Studio kuna karo (chemba) kutoka katika nyumba za hapo zinatoa kinyesi na maji yake ambayo yanasambaa mtaani na wala Wananchi hawajali lolote.
Jambo hilo baya kwa afya linaweka hatarini afya za Wakazi wa hapo ikiwemo kuwa hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza na magonjwa ya tumbo.
Moja ya swali ambalo tunajiuliza ni kuwa Mamlaka zimekuwa zikifungia Watu nyumba kwa sababu ya uchafu katika maeneo mengine kama Kilimahewa na Jang'ombe lakini kwanini nyumba hizo zinazoweka afya za Watu hatarini wamekuwa wakiziogopa?