Nyumba za polisi zateketea kwa moto Tanga

Nyumba za polisi zateketea kwa moto Tanga

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Moto mkubwa ambao bado chanzo chake hakijafahamika, umeteketeza nyumba za askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Msambweni, Mapinduzi A, Kata ya Ngamiani Kusini, Tanga.

Moto huo umeteketeza baadhi ya mali mbalimbali zilizokuwa ndani ya nyumba hizo, huku thamani ya mali zilizoharibiwa ikiwa bado haijafahamika.

Juhudi za kuzima moto huo zilifanyika kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi pamoja na wananchi, na kufanikiwa kuuzima kabla haujasambaa zaidi.
 
Back
Top Bottom