Nyumba Nafuuu
Katika eneo linalojitahidi hasa kwa vijana kuajiri ni hili la kuchora ramani. Congrats
Kuna mambo mnatakiwa kuyaboresha kwa ushauri tu.
Kwanza, msitazame nyumba kubwa kubwa, fikirieni pia nyumba ''nafuu'' kwa maana inayoweza kuhifadhi familia kulingana na kipato. Mfano, unaweza kufikiria nyumba ya ''vyumba 3'' kwa jicho la ku accomodate familia ndogo ikiwa na huduma zote.
Pili, fikirieni si kuwa na ramani tu, bali utaalamu wa maeneo mengine kwa kushirikiana
Mfano, ikiwa mnachora ramani, muweze pia kuwa na ushirika na Engineer, fundi bomba na umeme, na mafundi wa ujenzi wataalamu si wachanganya sementi tu ili makadirio yakitokayanakuwa ya jumla
Fikirieni '' town house'' n.k.
Tatu, mnaweza kuwa na ushirika na watengeneza matofali yenye ubora na kiwango
Hoja yangu kubwa ni kuwa gharama haziwezi kupimwa kwa matofali na mabati tu.
Mtu akipewa estimate ya milioni 10, 40, 60, 80 n.k. atakuwa katika nafasi ya kujiridhisha kuwa kiwango husika kitatosha katika maeneo yote na kwamba hatakuwa na sababu za kukimbizana na mafundi.
Siyo lazima mfanye ninyi kila kitu, muhimu ni kuwa na ''connection' za maana, kwamba, ubora wa ramani zenu uambatane na ubora wa vingine! kama utanielewa.
Hili litawezekana kama hamtakuwa wachoyo kwa ku sub contract kazi nyingine chini ya mwamvuli wenu! it's possible
Natamani sana kungekuwa na qualified and registered company za mafundi umeme, (Engineer na Technician), Plumbers na sewerage wanaojua kazi zao ili kutuepusha na vishoka.
Vijana hasa graduate na Technicians mlio na uzoefu mumefikiria haya?