Nyumba zilizopo kanda ya ziwa ni kama mapiramidi ya Egypt

Nyumba zilizopo kanda ya ziwa ni kama mapiramidi ya Egypt

Mapaa ya ukanda wa magharibi na kanda ya ziwa hatari tupu, na tatizo linaanzia kwa watu kujenga nyumba fupi na kulazimisha mapaa marefu
Mapaa ya kishamba sana haya. Inakuwaje paa liwe refu kupita urefu wa ukuta wa nyumba?
Ni sawa na mtu kuvaa kofia ndefuuuuuuuuuuuu kupita urefu wako.
 
Fikiria.

Msingi una kozi Tano za tofali ya nchi sita kutoka usawa wa ardhi, Kuna kozi nne za tofali then lenta (Ili uanze kukata madirisha) then tofali kozi Kumi au 11 alafu lenta Tena then anafunga kozi 4 au 5.....

Unadhani paa la hiyo nyumba litakuaje,????

Fikiria Tena wenzako wanaokuzunguka wamejenga nyumba za aina hiyo wewe utajenga ya aina gani?????
 
Huwa sipendi huu ujenzi basi tu ,kwangu sitojenga hivi,bati kubwa mno mpaka nyumba haionekani
 
Tunatafuta umaridadi

Ila napendelea na ukuta uwe mrefu
 
Hizi nyumba zinapendeza acheni utani kisa made in kanda ya ziwa.

Uezekaji wake wala siyo hatari. Wale vijana wake vizuri na wanapandisha kenchi ya kwanza na kuning'inia nayo kwa amani kabisa tofauti na unavyodai ni hatari. Kazi hii ina wenyewe.

Mtoa mada endelea na tembe na slope zenu za Dodoma na Singidani.
 
Ukutaka kushangaa zaidi nenda Geita, aiseeh yani nyumba fupi ula bati ni refu sana.

Mara nyingi nyumba hizi huwa zinazidiwa na uzito wa paa, unless iwe imejengwa vizuri.

Ndoo ndogo kumi za mchanga (zile za litre 10) kwa mfuko mmoja wa cement.
 
Kati ya mambo machache ya msingi Makonda aliwahi kusema nikakuta na mimi nilikuwa nawaza hivyo hivyo. Hii fasheni ni mbaya tangu naiona day one, nikamwambia mtu inakuwa kama mtu mwenye kichwa kidogo kavaa kofia kubwa.
Makonda alisema hii kitu hataki kuiona katika mkoa wake, lakini hapa Dar kuna watu wanafanya hii kitu pia[emoji38][emoji38].
 
Aisee ujenzi wa kanda ya ziwa unaweza kujiuliza yule fundi kafikaje juu ya paa.

Nyumba inajengwa vizuri ila upande wa kuweka bati ilibaki kidogo kuwa na usawa wa gorofa moja.

View attachment 2528266
Hivi hawa wanatumia tofari hizi hizi tunazotumia wengine au wao zao ni ndogo..maana mpaka lenta kuna kozi 15 pamoja na renta 2 harafu juu ya renta kuna kozi nyingine 5
 
Kupunguza joto, pia kule darini unaweza kufanya stoo, wazee wa Mbeya tukuyu walijenga sana hivyo zamani kule juu utakuta kuku wanalala kule kuna uhifadhi mahindi na kila aina ya mazao
 
Kupunguza joto, pia kule darini unaweza kufanya stoo, wazee wa Mbeya tukuyu walijenga sana hivyo zamani kule juu utakuta kuku wanalala kule kuna uhifadhi mahindi na kila aina ya mazao

Kwa mafundi wengine kule kwenye dali inawekwa hadi chumba cha kulala lakini hoja kubwa watu wajenge ukuta mrefu, msingi uwe mrefu na ukuta uwe mrefu pia hapo ndio nyumba inakua na muonekano mzuri
 
Angle ya mgongo wa paa kuwa kubwa, wala siyo shida, ila sema Designs zao ni mbaya...
Angalieni hizi
 

Attachments

  • images-44.jpeg
    images-44.jpeg
    13.7 KB · Views: 11
  • images-45.jpeg
    images-45.jpeg
    28.6 KB · Views: 12
  • images-46.jpeg
    images-46.jpeg
    66.9 KB · Views: 11
  • images-47.jpeg
    images-47.jpeg
    45.4 KB · Views: 13
Back
Top Bottom