Nyumbani kwa Clement Mohamed mtamila ndipo ulipotoka uamuzi wa julius nyerere kuacha kazi ya ualimu

Nyumbani kwa Clement Mohamed mtamila ndipo ulipotoka uamuzi wa julius nyerere kuacha kazi ya ualimu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HAPA NDIPO ILIPOJADILIWA BARUA YA JULIUS NYERERE KUCHAGUA SIASA AU UALIMU

Hapo liliposimama jengo hilo ndipo ilipokuwa nyumba ya Clement Mohamed Mtamila katika miaka ya 1950 harakati za TANU kudai uhuru zilipopamba moto.

Huu ni Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Kleist Sykes) na unaokatiza ni Mtaa wa Sikukuu.

Mwaka wa 1955 Mzee Mtamila alikuwa Mwenyekiti wa TANU.
Wakati ule TANU ilikuwa na Rais na Mwenyekiti nafasi zilizoshikwa na Julius Nyerere na Mzee Mtamila.

Ilikuwa baada ya Nyerere kurejea kutoka UNO ndipo waajiri wake Wamishionari hawakuweza kumstahamilia wakamwambia achague siasa au kazi yake ya ualimu.

Mwalimu Nyerere aliamua kuacha ualimu akachagua siasa.

Mjadala wa Nyerere kuacha kazi na kuwa mtumishi wa TANU ulifanyika nyumbani kwa Mzee Mtamila hapo sasa ilipojengwa hilo ghorofa.

Katika wajumbe waliohudhuria kikao kile alikuwa Bi. Tatu bint Mzee.

Bi. Tatu bint Mzee alikuwa anaishi Kirk Street mtaa nyuma ya Mtaa wa Kipata.

Mtaa huu sasa unajulikana kama Mtaa wa Bi. Tatu bint Mzee.

Ingawa nyumba yenyewe ya asili ya Mzee Mtamila haipo lakini pangewekwa kibao cha kueleza historia hii muhimu ili ibaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Picha ya kwanza ilipokuwa nyumba ya Mzee Mtamila ya pili Msikiti wa Kipata na ya tatu Mtaa wa Kipata kama ulivyokuwa katika miaka ya 1970.

Picha ya mwisho inamuonyesha Mzee Mtamila wa kwanza kulia katika jukwaa na Julius Nyerere.




 
Historia ya ukombozi wa Tanganyika ina watu wengi muhimu bahati mbaya au makusudi wamefichwa hawatajwi,anatamba Nyerere tu au kwa kua wengi wao ni Waislamu?
 
Historia ya ukombozi wa Tanganyika ina watu wengi muhimu bahati mbaya au makusudi wamefichwa hawatajwi,anatamba Nyerere tu au kwa kua wengi wao ni Waislamu?
Chinga One,
Mwalimu Nyerere alikuwa na hamu kubwa sana kuwa historia ya kuundwa kwa chama cha TANU ianze na yeye.

Bahati mbaya historia ya TANU inaanza na historia ya African Asociation (AA) mwaka wa 1929 na ukoo wa Sykes mchango wao katika hilo ni mkubwa.

Kubwa zaidi ni kuwa historia hiyo iliandikwa na muasisi mwenyewe wa AA Mzee Kleist Sykes na wanae wote walishiriki katika AA na TANU na ndiyo waliompokea Nyerere.

Kuhusu Waislam na mchango wao hili hakuna asiyelitambua lakini imengia hofu.
 
Back
Top Bottom