NYUMBANI KWANZA:Filamu Bora Za kibongo!!!

Ntakasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2013
Posts
1,428
Reaction score
456
Swahibaz Mpooo?.
Haya ,list yangu ya movies bora za kukupa burudani kwa uzalendo hii hapa..
1.Fikra Zangu.
Ni moja kati ya movies za kibongo ambazo SITACHOKA kutazama ingawa kuna makosa ya kiufundi yaliokuwepo lakini hayakufunika uwezo wa vinara kama Jacob Stephen na Irene Paul pamoja na wengineo waliovaa vyema uhusika wako....kuna kaka ameigiza kama mmakonde alisaidia kwa kiasi kikubwa movie kunoga.

2.Kibajaji.
Kama hujawahi kuitazama basi ni movie ambayo najitolea kuipromote na kukusihi ununue ukae nayo nyumbani.....Sistaduu Irene Paul Kaigiza vizuri kama mke wa dereva kibajaji mwenye wivu akiwa sambamba na Mboto.

3.Apple
hii imeigizwa na Irene Uwoya,Patcho Mwamba,Juma Chikoka,Baba Haji na wengineo....
Pamoja na kwamba ilibuniwa kuwa ya kipelelezi ila cast walifanya kazi nzuri ya kuchangamsha movie na kuifanya iburudishe haswaa.

4.For My Child
Hii imeigizwa na Hemedi suleiman,Patcho Mwamba na Elizabeth Swinny......The best part ya hii movie ni mtoto ambaye jina lake limenitoka alivyoweza kuigiza kwa ustadi akiwa anahangaika na baba yake na baadae kumtetea kwa nguvu mahakamani.

5.Tikisa
Hii ni comedy na kama tunavyomjua Mzee Majuto huwa hakosei na uzuri wa hii movie ni mchanganyiko wa personalities za wahusika kama Hemed suleiman,Haji Mboto,Salma Jabu Nisha,Jackline Wolper,Chuchu Hans Na Mzee TIKISA mwenyewe...King Majuto.

6.Safari
Single Mtambalike pamoja na Irene Uwoya na Kaka aliyeigiza kama mmakonde kwenye Fikra Zangu Walifanya kazi nzuri sana pamoja na kwamba ilikuwa inatisha lakini cast ya kijijini iliifanya isisimue na kuleta maana mwisho wa siku....walisindikizwa na Chuchu Hans pamoja na Msuya

7.Uyoga
Wakongwe walikutana na kufanya kitu kizuri pamoja.
Namzungumzia Yvonne Cherly na Single Mtambalike wakisaidiwa na Simon(Rado),Sudi na Flora Mvungi...Ni movie inayohusisha tukio la siku moja na uyoga uliodhaniwa kuwa na sumu uliowafanya watubu makosa yao wakijua wanakufa kumbe walaaa!

8.Waves Of Sorrow
Hii ni production ya RJ ambao walimrudisha tena Batuli wa Kanumba(Yobnesh Yusuph) kwenye chat humu...Akiwa sambamba na Rose Ndauka,Vincent Kigosi na Slim Omary...Story iko clishay yaani ni common sana ila Batuli aliweza kuvaa uhusika mzuri na kufanya ivutie.

9.Bad Luck
Hii ni mpya mpya na imemshirikisha Salha Israel aliyewahi kuwa Miss Tanzania akiwa na Blandina Chagula,Esha Buheti ,Haji Adam,Abdallah Ambua na Yobnesh Yusuph bila kumsahau Slim Omary....ina kisa
kizuri na wameigiza vizuri sana.

10.Stella
Hemed amemshirikisha dada chipukizi ambaye amefanya vizuri sana...Getrude wakiwa sambamba na Gelly wa Rhymez...na hii ni mpya mpya sokoni waweza kupata copy yako.

ANGALIZO:
Nzuri zipo nyingi ila nimekwepa zile za marehemu Kanumba ili kuwapa nafasi na wengine kuwika na kusongesha gurudumu la kiwanda cha filamu TANZANIA.
Pia inasikitisha kuona chipukizi wakiwa hawafurukuti na hii sio sababu hawapewi tafu tu bali pia kazi za chipukizi wa filamu nyingi za sasa ni Mbovu Mnoooo na HAZITAZAMIKI.....Ni wachache sana wanaojitahidi...
Ahsanteni.
 
STELLA ni kali vibay mwanzoni sikumuelewa yule dada aliyeigiza kama stella but dah kafanya wonders mule,safi sana pongezi kwa director kwa kumbadilisha hemed suleiman nae kafanya poa sana mule,TIKISA is the best comedy nisha naye kajitahid sana mule,nilipenda mwisho alivyocheza pamoja na uchizi wake wote ila alishindw kuvumilia kumpoteza mumuwe hemed kwa wolper,it was good alivyokuw anaongea kwa uchungu ingaw ilikuw kind of comedy iko super,izo nyingine sijaziona,kuna hii movie inaitwa WHITCH DOCTOR ya odama dah huyu dada kuna kitu cha ziada na cha kipekee anacho,ukiichek lazima uondoke nayo moyon yaan unaiwazia haitok akilin kirahis inakuacha na maswal mengi kuliko majibu,uwaga sina mashak kabisa na huy dada
 
Na kuna hii movie inaitwa MATILDA dah yule sista duu kakamua vibaya mule,ingawa alikuw underground ila kwa kiwango alichoonyesha duh hatar tupu,kanaitwa UWERU SENGO sijui,dah hii movie ilikosaga promo ya maana but one the hot movie,cast ilishiba,hemed as usual,ni kali Dana
 
Odama anaweza pia,umenikumbusha aliigiza na Hemed.....kwenye HOUSEMAID....ILIKUWA BOMBA SANA...hiyo WITCH DOCTOR nitaitafuta.....
 

Haaahaaa anaitwa Wellu Sengu yule...ana shepu ya hatari pia hata hivyo anajitahidi vilevile....
 
She is such a gorgeous girl,kako vizur,halafu anajua kuutumia mwil wake na uzur wake kwenye camera basi dah anaonekana bomba sana,apa akina wema wanasubir sana
 
Kibajaji moto sana! Mboto hajawah kosea na irene paul huyu mdada ni levo za mbefele kabsa!
 
if someone may speak out loudly what is she/hea learning from these bongo movies I will certainly start watching them from now on

so far I know they meant for LOW MINDED PEOPLE, DUMP, waste, people who know nothing about the other world of movies

''no food for thought'
 
Duh siangaliia bongo movie,kama uangaliag bongo movie ata hii thread usingefungua,si uliona heading ni kuhus bongo movie?? Ungetumia busara zaidi ya kukaa kimya na kupita kama wengine,apa tunajadiliana maada mbalimbali na sio maada zoote lazima ziwe ni interest yako,umeona hapakufai chapisha makalio out,mijitu mingine bhna imezoea kutoa maneno mbofu mbofu tu
 

"People who are quick to judge the status of others are not what they think they are"-Ntakasi
Not liking these movies is one thing but judging others just because they are patriotic enough to care about their own stuffs is another issue!!
 
APPLE kali sana,niliiangalia nikarudia tena na bado sijaichoka.
 
Kibongobongo mnaweza mkazisifia maana hata kati ya wabaya mzuri yumo, but kwa level za kimataifa hizo zote ni pumba kabisaaaaaaaa!!
 
basi sawa ngoja nijaribu na mimi kuziangalia maana nliacha kuzitizama movie za kibongo miaka mi2 iliyopita kutokana na kuchoshwa na vituko kama"jambazi anavamia nyumba uku akiwa mpeku! apo viatu amevua asichafue nyumba ya watu" mzimu unavuka barabara huku unaangalia kushoto na kulia! mtu anaamka asubuhi ukimwangalia unaona ma wanja na mapouda n.k.. eti ngoja niwaulize swali hivi bado scenes zao zinaonesha"jumba zuri,ofisini, beach na gari tu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…