Nyumbani ni nyumbani hata kama ni kichakani

Nyumbani ni nyumbani hata kama ni kichakani

Sijui msemo huu unaendana?

Nakumbuka kuna siku nimetoka shule sijavua hata uniform nikaambiwa nikafungue ng'ombe zilipofungwa kwa malisho nizirudishe nyumbani kufika pale(kipori Fulani) badala ya kufungua kamba niswage ng'ombe nikakimbilia kichaka kilikuwa na matunda pori(mang'ang'a wanyakyu wanaelewa) .Bhanabhana...kumbe pembeni kuna nyuki wa haja ile napeleka mkono tu kushika majani kumbe nimewatikisa😳

Nilitoka mbio,lakini kumbe nilikuwa nimechelewa walining'ata sana macho,pua,mdomo,masikio na kisogo😏.....ndo hivyo bhana lakini pamoja na kuvimba kote na macho kujifunika kwa mvimbo niliweza kupapasa njia mpaka nikafika nyumbani.

Kilichonifanya nijue nimefika ni vicheko nilivyopona wakasema walivyoniona tu walishindwa kujizuia kucheka(nadhani mwonekano baada ya kuumuka)

Nyumbani ni nyumban
Siyo lazima upost
 
😂😂nyuki bhana waliniuma jichoni likavimba nikawa sioni naona jichomoja alafu kunafala akanipigia video call whatsaap 😀 nikapokea alinicheka balaa 😂😂
😂😂😂mi nisingepokea aisee
 
Nyumbani ni Nyumbani, nakumbuka sisi tukifanya zali au tukio lolote likitokea ni nduki hadi home, hakuna kuuliza, kuna siku nimepanda mti wa zambarau kumbe juu kuna finyofinyo, alooo niliwashwa breki ya kwanza home sielewi moja kwa moja bafuni najisungua naskia mwili unawaka moto balaa😂😅
 
Kwa kweli hapo enzi hizo nyumbani angali tukiwa machalii basi tulikua na kijitabia flan hivi mimi na wenzangu wawili tukitoka shule kurudi nyumbani tunakutana kituoni na kuongozana basi tukiwa njiani tulikua na visanga vingi sana tunavifanya moja wapo ilikua kuchezea kengele za watu kwenye nyumba zao, Sasa kulikua na nyumba moja bwana aah! hiyo tuliipenda kuionea sana yani kila tukifika hapo ilikua lazima tuibofye kengele tena zamu kwa zamu, Ila siku moja ilikua bahati mbaya yetu hatukujua kumbe wenyewe walikua wamefungulia mbwa bwana dah! Ilikua hatari ile rafiki yangu kabofya tu weeeh! Kifaa hichi hapa mbele yetu halafu alikua ni German Shepherd 🐺 hahahaa 😂😂😂 hapo kila mmoja na njia yake nakumbuka nilifika nyumbani nikiwa vumbi mtu huku nimeshikilia mkono wa kushoto ukiwa umeteguka lakini haikutosha kuwa sababu kwa mama kunielewa haraka kwakua nilikua mtundu sana nilichezea kichapo kisha ndio nikapelekwa hospitali baada ya siku tatu nakuja kuonana na jamaa zangu ilikua nivicheko tuu maana mwenzetu mmoja alitumbukia kwenye shimo la taka na kuchanwa na chupa mguuni..
 
Back
Top Bottom