Nyumbani ni nyumbani hata kama ni kichakani

Siyo lazima upost
 
πŸ˜‚πŸ˜‚nyuki bhana waliniuma jichoni likavimba nikawa sioni naona jichomoja alafu kunafala akanipigia video call whatsaap πŸ˜€ nikapokea alinicheka balaa πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚mi nisingepokea aisee
 
Nyumbani ni Nyumbani, nakumbuka sisi tukifanya zali au tukio lolote likitokea ni nduki hadi home, hakuna kuuliza, kuna siku nimepanda mti wa zambarau kumbe juu kuna finyofinyo, alooo niliwashwa breki ya kwanza home sielewi moja kwa moja bafuni najisungua naskia mwili unawaka moto balaaπŸ˜‚πŸ˜…
 
Kwa kweli hapo enzi hizo nyumbani angali tukiwa machalii basi tulikua na kijitabia flan hivi mimi na wenzangu wawili tukitoka shule kurudi nyumbani tunakutana kituoni na kuongozana basi tukiwa njiani tulikua na visanga vingi sana tunavifanya moja wapo ilikua kuchezea kengele za watu kwenye nyumba zao, Sasa kulikua na nyumba moja bwana aah! hiyo tuliipenda kuionea sana yani kila tukifika hapo ilikua lazima tuibofye kengele tena zamu kwa zamu, Ila siku moja ilikua bahati mbaya yetu hatukujua kumbe wenyewe walikua wamefungulia mbwa bwana dah! Ilikua hatari ile rafiki yangu kabofya tu weeeh! Kifaa hichi hapa mbele yetu halafu alikua ni German Shepherd 🐺 hahahaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hapo kila mmoja na njia yake nakumbuka nilifika nyumbani nikiwa vumbi mtu huku nimeshikilia mkono wa kushoto ukiwa umeteguka lakini haikutosha kuwa sababu kwa mama kunielewa haraka kwakua nilikua mtundu sana nilichezea kichapo kisha ndio nikapelekwa hospitali baada ya siku tatu nakuja kuonana na jamaa zangu ilikua nivicheko tuu maana mwenzetu mmoja alitumbukia kwenye shimo la taka na kuchanwa na chupa mguuni..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…