Nyumbu 20 waangushwa kuwanasa Wahadzabe kuhesabiwa

John Walter

Member
Joined
Aug 14, 2017
Posts
68
Reaction score
63
IMG_5848.JPG

Na John Walter-Manyara

Serikali ya Tanzania imetoa wanyamapori 20 aina ya Nyumbu kwa jamii ya Wahadzabe ikiwa ni sehemu ya takwa lao ili wawe tayari kushiriki zoezi la Sensa linaloanza usiku wa kuamkia Agosti 23 hadi Agosti 31 mwaka huu.

Sensa ya mwaka huu inafanyika kwa mara ya sita ambapo hufanyika kila baada ya miaka kumi.

Jamii ya Wahadzabe ni miongoni mwa makabila machache nchini Tanzania yanayoendeleza mila na desturi wakiishi Zaidi kwa kutumia uwindaji na kuokota matunda ambapo katika matukio muhimu ya serikali hulazimika kutumia mbinu mbadala ili kuweza kuwaweka pamoja na kuhudumiwa.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere akikabidhi nyama hiyo kwa Wahadzabe katika kijiji cha Mongowa Mono amesema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kupata idadi kamili ya wananchi wote katika maeneo yote nchini ili kuweza kupeleka huduma za kijamii kulingana na idadi ya watu.

Hata hivyo jamii hiyo ya wawindaji licha ya kuishukuru serikali kwa kuwapatia nyama hiyo,wameiomba serikali iwapatie ndege aina ya Mbuni kwa madai kuwa wanatumia Manyoya yake kwa ajili ya dawa na matambiko yao.

Kwa kuonyesha kufurahishwa kwao, Wahadzabe hao wamempa zawadi ya asali lita 20 mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere na lita 10 mkuu wa wilaya ya Mbulu Sezaria Makotha.
 
Hao jamaa siyo sensa hii tu. Hata Ile iliyopita ya mwaka 2012 pia waliweka sharti hilo hilo la kupewa nyama pori ili wahesabiwe. Ni kama vile Kila ikitokea shughuli ya serikali inayo wahusu wao pia ni lazima waweke sharti hilo ili washiriki.
 
Ndugu hawa jamaa ni tofauti na viwanaume vya Dar.. wale kila siku lazima watoke kuwinda ili wapate mlo wa siku hiyo...kwa hiyo ili wasitoke waletee menyu
 
Hao jamaa siyo sensa hii tu. Hata Ile iliyopita ya mwaka 2012 pia waliweka sharti hilo hilo la kupewa nyama pori ili wahesabiwe. Ni kama vile Kila ikitokea shughuli ya serikali inayo wahusu wao pia ni lazima waweke sharti hilo ili washiriki.
Wanaakili sana na hawana utani na ubrand wao

Lini unaweza taka kumuhoji 50 cent na usimlipe au jay z ,wao maisha yao hawahitaji serikali wanahtaji mapori na nyama
 
mie mewaza kiafya kubeba wale wanyama kwenye lori kwa namna ile ni sawa? pia hata walivyowekwa hapo chini hivyo.

Ingalikuwa vyema kuwachukua wazee na vijana wa kabila hilo, kwenda nao sehemu walipowinda na kila anayeuliwa anatolewa ngozi na kuwaandaa vizuri
 
Haina shida.
 
Hao jamaa siyo sensa hii tu. Hata Ile iliyopita ya mwaka 2012 pia waliweka sharti hilo hilo la kupewa nyama pori ili wahesabiwe. Ni kama vile Kila ikitokea shughuli ya serikali inayo wahusu wao pia ni lazima waweke sharti hilo ili washiriki.
Inaelekea wanahusudu sana nyama
 
mie mewaza kiafya kubeba wale wanyama kwenye lori kwa namna ile ni sawa? pia hata walivyowekwa hapo chini hivyo.

Ingalikuwa vyema kuwachukua wazee na vijana wa kabila hilo, kwenda nao sehemu walipowinda na kila anayeuliwa anatolewa ngozi na kuwaandaa vizuri
Hakuna tatizo
 
Nasikia hao jamaa walipanda nyama[emoji39] ili iote ya kweli ayo wandugu
 
Back
Top Bottom