Nyuzi za namna hii zimekuwa nyingi mno, kulikoni?

Nyuzi za namna hii zimekuwa nyingi mno, kulikoni?

100 others

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2017
Posts
4,766
Reaction score
16,191
Hizi nyuzi za namna hii zimekuwa nyingi sana, ni muda mrefu sasa lakini this time imekua too much. je umekutana na nyuzi za namna hii au zinazorandana na hizi za kusifu na kuabudu ujinga?

Tanzania yawa nchi ya mfano Africa.....blah... blah.... blah....

Tanzania Yashika Namba 4 Kati ya Nchi 10 Zenye Uchumi Imara 2022​


Tanzania yatajwa kuwa Nchi Bora ya Kufanya Uwekezaji na Biashara Afrika, yashika namba 11​

Tanzania yavunja rekodi kwa kupata watalii wengi .....blah....blah....

Walivyo waongo sasa siku treni zikianza kufanya kazi na tatizo la umeme kupungua kitu ambacho ni ujinga kujisifu kwa nchi yenye umri wa miaka 61... utasikia

Tanzania yashika nafasi ya pili duniani kutokomeza tatizo la umeme

Siku treni zikianza kufanya kazi maroboti yatakuja tena hapa, yashasetiwa

Tanzania nchi ya kwanza Africa kumiliki treni zenye AC na nchi ya 5 duniani. 😂🤣

Baada ya popoma hao kuanzisha uzi, wanafuata chawa sasa wazee wa kusifu.. hapo utasikia, Hakuna kama mama, nani kama mamaaa!!. chawa jingine linafuatia na kumreply chawa namba 1 hakunaaaa


Hizo nyuzi tumechoka mazeee.... Hivi why mnatumia nguvu sana kufanya kampeni..

Mnachokosea ni kwamba, wananchi wanataka kuona kazi, watu wanataka kuona vitendo dhidi ya maneno, habari za jarida la forbes sijui limeenda likarudi likakusanya takwimu watu hawataki hizo habari.

Nasubiri maroboti yaliyoprogramiwa kuwaita watu Sukuma Gang yaje.....
 
Back
Top Bottom