alma gemela
JF-Expert Member
- Feb 22, 2013
- 842
- 280
Kuna imani wanajiita waaminio hawa mwanamke hanyoi nywele kaka angu binti zake hawakatwi nywele za utoto wanakuwa nazo wana nywele refu sana sasa sijui wanaungana na nini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili nitalitafiti
Hiyo inategemeana na Chuo kinahusiana na nini?,mfano tulipokuwa sekondari walitukataza kufuga nywele na ndevu,sasa je nako ni ushirikina?,Ukienda Polisi na majeshi mengine nywele hairuhusiwi kufuga je nako ni ushirikina?,Ipo cku mtawahusisha watu wanaopenda kunyoa nywele zao mara kwa mara na ushirikina wakati ndiyo ustaarabu wao uko hivyo.
Ni kumi kwa moja halafu asilimia kubwa ni hiki kizazi chetu wazee wa zamani huthubutu kumuacha mtoto na nywele alizotoka nazo tumboni
Hii sabrinah..
Mara nyingi kiimani nywele za mtoto mchanga zinanguvu sana katika mambo ya kichawi. Mara nyingi nywele huashiria ufahamu wa mtoto. Zamani wengi nywele zilichukuliwa na kufanyiwa mila au matambiko. Kufanya hivyo unamfunga mtoto ufahamu wake unamkabidhi over the other side. Si lazima kumnyoa mtoto nyewele zake na hata zikinyolewa zikatupwe mahali mtu mbaya haezi fukia.
mfano mchawi anapomnyoa mtoto hata wa secondary nywele anaweza kuhamisha ufahamu wake na akili yake kwa mtu mwingine ndipo unaanza kusema mtoto amekuwa mjinga ghaflaa au ameanza kufeli ghaflaa tu. Ukiona hivyo jua kuna jambo.
Tukienda nje ya mada kitovu nacho huashiri uhai wa mtu na nafsi yake wengi wamefungwa kozi vitovu vilifanyiwa mila. So ni vyema kumnyoa mtoto mwenye na kitovu chake ukipe mwenye baada ya kukuombea.
Mkuu tangaza nia!!Kuna mambo ya kushangaza ambayo kwasababu ileile ya kimapokeo na mazoea huwa hatuyahoji au hatuna muda wa kufuatilia na pengine tunaridhika tu na hivyo yalivyo.
Nywele hizi zetu za kichwani zinabeba siri kubwa ambayo ina mawasiliano ya moja kwa moja na kuzimu au na roho zinazotangatanga.
Hebu tujihoji haya;
- Kwanini baadhi ya imani ni marufuku na hairuhusiwi kwa mwanamke kuonyesha nywele zake hadharani?
- Kwanini mchawi/mwanga anapokamatwa hukatwa nywele zote ili kummaliza nguvu zake?
- Kwanini chizi kichaa au mwendawazimu hunyolewa nywele kama sehemu ya tiba?
- Kwanini wachawi na waganga wengi hutumia nywele kama sehemu ya uchawi/ulozi wao?
Historia ya nywele kuhusiana na roho na nguvu za kiza inaanzia mbali sana miaka elfu nyingi iliyopita kwenye habari za Biblia takatifu kisa cha Samsoni na Delilah pale Mwenyezi Mungu alipoweka nguvu isiyomithilika kwenye nywele za Samsoni lakini shetani kupitia Delilah alimrubuni Samsoni na Samsoni akatoa siri ya nguvu zake.
Ni kutoka hapo ile nguvu ya kimungu iliyowekwa kwenye nywele za Samsoni iligeuka na kuwa nguvu ya kishetani na kufanya maangamizi makubwa, tangu hapo nywele imekuwa ni kitu kinachohusishwa na roho chafu na mapepo.
Hapo nimekupata ila kwa sasa sijui kama kuna anaeamini haya maana hata ule mvuje anaovalishwa mtoto kuepusha kushituka watu wakimuona unaambiwa mvue mtoto hirizi
Ndomaana nivizuri baada ya kunyoa nywele uzichimbie na kuzifukia, ila kabla unatakiwa uangalie kushoto na kulia kama kuna anaye kuona. Kama hayupo fukia kisha sepa!!
Roho zinazo tangatanga zinakuona, usidhani unaweza kujilinda mwenyewe, huna huo ujanja (only God can..) mara nyingi umeacha nywele zako saloon wakati hata kinyozi humjui..
uko sahihi sana,kwanzi leo nikienda soloon kunyoa wakimaliza tu naondoka na nywele zangu-maamuzi magum
Hahahahhahaha yani wewe umeua band
Sio nywele tu...
Kitu chochote kinachotoka mwilini mwako kinakuwa kimebeba DNA yako...
DNA ni kama formula ya mwili wako, ni sawa na hackers wabebe system file la program yako...
Wachawi ni hackers ambao wanahack DNA system yako...