Mbaga Jr
JF-Expert Member
- May 28, 2018
- 29,028
- 69,666
Kitambulisho cha nida hakipigi kura.Wife juzi kanipgia simu kuniambia kuna watu wamekuja home hapa Nzega mjini, kata ya Nzega Mashariki, Mtaa wa Buswiru wanagawa mitungi ya gas bure nikamkatalia kuchukua.
Sasa Leo ikabidi nimdodose yaani ni kina nani mpaka wagawe gasi bure, akasema wao wakishakupa gas yao wewe unawapa namba yako ya NIDA hapo tayari wanakuwa na uhakika wa kura yako mwezi Oktoba.
Wakuu hii inawezekanaje si rushwa hii? Na kaya nyingi sana zilizofuzu vigezo hivyo zimechukua mitungi
Kuna uhusiano gn wa hy namba ya nida na kupiga kura?