Nzi akiacha ujinga anaweza kutengeneza asali, hongera Paul Makonda

Nzi akiacha ujinga anaweza kutengeneza asali, hongera Paul Makonda

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Habari za wakati huu;

Ni matumaini yangu kwamba mnaendelea vyema na majukumu yenu ya Ujenzi wa Taifa letu hili tukufu la Tanzania. Kwa wale ambao wanaifahamu Siasa sidhani kama hili la Paul Makonda kuwa Mwenezi wa Chama ni Jipya na la kushangaza kwao. Actually, kama wakisoma alama za nyakati vizuri basi wataona kwamba uelekeo ni kwamba kuna mabadilko yanaendelea.

Najua kichwa cha mada yangu kina sauti ya kejeli ila sio lengo la mada hii kukejeli bali nataka tujadili katika misingi ya maslahi mapana ya nchi,chama na serikali.Katika Nchi yetu,Chama Ndio kinashika hatamu.

Katika Siasa za Nchi yetu Paul Makonda Alifika katika hatua ya kisiasa ambayo kwanza ilimjengea profile kubwa, ilimjengea maadui na ilimjengea marafiki. Ila ni ukweli usiopingika kwamba Yeye Binafsi alibeba sifa za aina ya viongozi ambao Watanzania wanawapenda, wanawahitaji na ambao wanawafaa watanzania. Viongozi ambao wanajua Fitna, wanaweza unafiki,wanaweza kusimami kile wanachokiamni na hata kama wamekosea wana uwezo wa kushawishi kwamba wao wako sahihi.

Changamoto aliyokuwa nayo Paul haikuwa kubwa na wala anguko lake la kisiasa halikuwa kubwa.Hata hivyo alichofanya baada ya kutoka kwenye Mfumo kilimtofautisha. Tetesi zinasema kwamba Alirudi shuleni kuongeza Maarifa. Alikaa kwa nyuma akiendeleza harakati zake binafsi za kisiasa huku akijaribu kwa kiwango kikubwa kutokuwa kwenye Lime light. Subira na Upole wake pamoja na changamoto za kisiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi zikatengeneza nafasi ambayo kimsingi inaweza kumpa Paul Makonda nafasi ya ama kujijenga zaidi ndani ya chama na serikali au kujibomoa zaidi ndani ya Chama na serikali

Kama nilivoeleza katika kichwa cha mada hii kwamba Nzi akitulia anaweza kutengeneza Asali,Basi nihitimishe kwa kusema kwamba Cmrd Paul Makonda Akituliza Kichwa chake sasa hivi Anaweza kuleta mabadiliko makubwa katika siasa za nchi ndani na nje ya chama.

Aaachane na kasumba kama zile za kuwakosema heshima watu,kujikweza kupitiliza na zaidi unapopanda Juu Usivunje ngazi ulizopitia maana ndio utazitumia kushuka chini.

Nakutakia kila la heri katika utumishi wako
 
Inzi ni inzi tu, na kamwe milele yote hawezi tengeneza asali, atabakia kutengeneza funza wanao ozesha taka na kutoa harufu mbaya sana za uozo

Ni watu wasio waza vema kufikiri chui atageuka kondoo na kuishi na kondoo, kamwe hilo haliwezekani, malaika atabakia malaika na shetani atabakia shetani, ndivyo enzi na enzi ilivyokuwa na itaendelea kukuwa hivyo, fikira fupi ni hatari sana dunia hii.

Mtu mchafu ni mchafu na tabia yake itaendelea kuwa uchafu, aliyezoea kuharibu hawezi kuendelea kujenga, na Mungu wetu tusaidie, muda sio mrefu utajua nasema nini, eti Makonda awe mwanasiasa mkubwa ndani na nje ya nchi, watu mnaumwa hysteria sana.
 
Sawa Mkuu! Nadhani amejifunza kutokana na makosa.

Hata kama skandali za vyeti zilikuwa ndiyo moja ya sababu zilizochangia kushusha hadhi yake, lakini kisiasa alikuwa bado yuko vizuri sana! Ni msemaji mzuri sana!

Na anaweza hata sasa!
 
Back
Top Bottom