Nzige wakiwa ndani ya eneo la Kilometa ya mraba 1, wanakula chakula cha kuwatosha watu 35,000 kwa siku

Nzige wakiwa ndani ya eneo la Kilometa ya mraba 1, wanakula chakula cha kuwatosha watu 35,000 kwa siku

Huku tuna jeshi imara, hata kwenye korosho jeshi lilitumika
 
Mpaka yawepo.

Tanzania hata majani yetu tuliyonayo hayawezi kulisha watu 35000 kwa eka licha ya mazao tunayokula. In fact hayawezi kulisha hata ng'ombe 1000 tu.

"Analysis" zingine hazina uhalisia.
We sema tu nyanya zimeadimika na nzige wakijakutua kwenye kisamvu si ndio tutanza kupanda majukwaani na kusema wakati naomba kura nilisema mimi nitaleta nzige!
 
Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA, Bwana Mark Lowcock amesema “wimbi moja la nzige waliozingira ukubwa wa kilometa moja , ambalo linajumuisha nzige milioni 40-milioni 80, wanaweza kula kwa siku moja chakula ambacho kinatosheleza kulisha watu 35000”

Akitolea mfano uvamizi wa nzige hao Kaskazini Mashariki mwa Kenya amesema wimbi la nzige lilikadiriwa kuwa ni la ukubwa wa kilometa za mraba 2, 400 na nzige hao wanaweza kula chakula ambacho kinaweza kulisha watu milioni 84 kwa siku

Wimbi la nzige limevamia Pembe ya Afrika ambayo tayari ina changamoto zingine kama ukame, njaa Somalia na Sudan Kusini, mafuriko na machafuko yanayoendelea hivyo imekuwa janga baada ya janga

Na watu milioni 30 hawana uhakika wa chakula kwenye maeneo ambayo yamekumbwa na majanga hayo.

Pia amesema katika saa 24 zilizopita wimbi la nzige limevuka mpaka na kuingia Uganda. Ameongeza kuwa “Kama mjuavyo nzinge ni wadudu wa kale sana ambao uhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na uvamizi wao unaweza kusambaratisha kabisa mazao na malisho haraka sana.”

Amesema “nzige hao sio tu kwamba wana njaa lakini wanasafiri haraka sana, nzige hao hawahusiki na masuala ya uhamiaji, au kuhitaji pasi za kusafiria na wala hawaheshimu mipaka ya kimataifa . Hili ni tatizo la kikanda na tayari tumepokea tarifa za uharibifu mkubwa wa mazao na mimea katika kanda hiyo.”


Chanzo: UN Swahili

The toughest test to Magufuli yet

Tuone atatumia akili gani to overcome this

You will how light these ccm bandwagoners are!
 
Back
Top Bottom