Sababu zipo kadhaa na chache zikiwemo za kihistoria, kimfumo, kitakwimu, na kijamii. Kihistoria - watu weusi walikandamizwa kutokana na hali yao ya kitumwa ambapo hawakuhesabiwa kama binadamu bali walihesabiwa kama mali. Kimfumo - sheria za kibaguzi kama za Jim Crow ambazo ziliwakandamiza watu weusi kwa kuwanyima elimu na mambo mengine ya msingi. Kitakwimu - idadi ya watu weusi wachache sana kulinganisha na watu weupe. Kijamii - watu weusi nao wao kwa wao wana matatizo yao. Kwa mfano, mtoto mweusi anayefanya vizuri darasani huwa anaonekana eti 'ana act white' kisa tu yuko makini katika elimu. Labels kama hizo huvunja mioyo ya watu wengi na hivyo kufanya jamii kwa ujumla wake kukosa mafanikio.
Uchaguzi wa mwaka huu uko tofauti sana na chaguzi za miaka ilopita. Hilo ni kwa sababu mgombea mdhaniwa wa chama kimoja, cha Republican, siyo mwanasiasa.
Donald Trump anaweza kabisa kushinda [ingawa binafsi sidhani kama atashinda]. Itakuwa ni jambo la kipumbavu kabisa kumpuuza. Toka alipotangaza nia wale wote waliompuuza imewatokea puani.
Kuhusu kauli zake tata hususan hiyo unayosema ya "kupiga marufuku waislam kuingia Marekani", kwanza, si sahihi. Trump hajasema anataka kupiga marufuku Waislam kuingia Marekani. Alichosema ni kwamba, wasitishe kwa muda kuruhusu wahamiaji na wakimbizi wanaotoka kwenye nchi za Kiislamu hadi hapo watakapokuja na njia iliyo bora zaidi ya kuwachunguza hao wahamiaji na wakimbizi.
Sasa kusitisha jambo kwa muda si sawa na kulipiga marufuku kabisa. Au wewe unaona ni kitu kilekile tu?
Pili, kuhusu kauli zake zingine za utata hususan kuhusu Afrika na Waafrika, hizo hazina ukweli wowote kwa maana ya kwamba hajawahi kuzitoa. Ni uzushi tu.
Labda kusimamia kuurudisha uchumi katika mstari baada ya mtikisiko wa 2008.
Ni imani potofu tu. Mafanikio hayaji tu hivi hivi. Mafanikio huwa ni matokeo ya fursa na uchapa kazi. Sasa, ukweli ni kwamba Marekani fursa zipo nyingi mno kulinganisha na Afrika. Lakini mtu usipochapa kazi huwezi kufanikiwa hata kidogo. Na uchapa kazi ni kanuni ambayo inatumika popote pale ulimwenguni.
Binafsi siupendi ushoga. Lakini pia naamini katika uhuru wa watu kufanya yale kitu roho inapenda ili mradi tu hawaingilii anga zangu. Hivyo, kama mtu ni shoga hayo ni mambo yake. Mimi hayanihusu. Kauli mbiu yangu ni 'fanya yako, ishi kivyako'. Mtu anajifanyia mambo yake kivyake, mimi inanihusu nini? Kwa nini nihemuke na mambo ya wengine? Tigo si zao? Sasa kama ni zao na wanapenda ziliwe, mimi inanihusu nini? Hainihusu.
Kwa jinsi changamoto zilivyo nyingi, sidhani kama nitakuwa na kipaumbele kimoja tu. Ila kilicho cha msingi zaidi ni utawala wa kisheria. Kwa hiyo nitaanza na hilo kwanza. Kuhakikisha nchi inatawaliwa kwa sheria na si vinginevyo.