Obama aichafua Kenya...

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,040
Reaction score
7,303
Rais Obama leo ameifananisha Kenya na Syria.

Amefafanya hivyo alipokuwa akitoa maelezo juu ya kazi ngumu zinazofanywa na waandishi wa habari wa Marekani.

Amekaririwa akisema "They've risked everything to bring us stories from places like Syria and Kenya, stories that need to be told".

Haijaeleweka kwanini Obama ameifananisha Kenya na Syria, lakini kauli hiyo imechukuliwa na wakenya wengi waliochangia maoni kwenye mtandao kuwa ni kuichafua Kenya na kutaka kuingilia mambo ya ndani ya Kenya.

My take: Wamarekani huwa waangalifu sana kwenye kuchagua maneno ya kuzungumza na hawasemi jambo bila kulichuja. Kwenye kauli hii kuna ujumbe juu ya position itakayopewa serikali ya Kenyatta na serikali ya Marekani.

Source: Kenya not safe for foreign journalists, says Obama - News - nation.co.ke
 
Inaweza kuwa tricks za kuinfluence kesi ya Raila ya uchaguzi. Sasa naanza kuhisi hii kesi kama ikifunguliwa inaweza kuwa na uzito mkubwa kuliko nilivyodhani awali!!!
 
...Mpuuzi tu..

Wamenifurahisha wakenya kwenye comments zao mpaka wale wenye majina ya kijaluo wamechukizwa na kauli hii ya Obama.

Inawezekana Obama pia alikuwa na matumaini makubwa kuwa binamu yake anaingia Ikulu ili wathibitishe kuwa wana super DNA...
 
Wakenya sasa wataijua vizuri Marekani. Kuna hatihati uchumi wa Kenya kuyumba. Kadhalika kuna uwezekano Kenyatta kutomaliza muhula wake, au kutumikia muhula mmoja. Ndoto za Raila kuwa Rais bado zipo.
 
Wakenya sasa wataijua vizuri Marekani. Kuna hatihati uchumi wa Kenya kuyumba. Kadhalika kuna uwezekano Kenyatta kutomaliza muhula wake, au kutumikia muhula mmoja. Ndoto za Raila kuwa Rais bado zipo.

Ila Obama akifanya mchezo wale al shabab wanaweza kuwa na free heaven pale somalia. Jamaa anaweza kuacha al qaida wawekeze mizizi kwenye horn of Africa...
 
Huyu nae Shoga! nani asiejua alikua side ya jaluo mwenzake Raila Odinga? Nadhani Kenya sasa ndo wakati wakujitoa ktk ukoloni huu wa US/UK...kwani tumesikia ata kauli ya baloz wa UK nchini Kenya na kauli yake Tata dhidi Ya UhuRu... Kenya lazima ijisimamie hasa kwani raia wa Kenya ndo wanamamlaka juu ya mustakabali wao
 
Jamani mbona yuko sahihi. Kule kaskazini mashariki Garissa kuna waandishi wa habari walitekwa. Mombasa na Lamu inabidi waingie kuripoti kimahesabu. Akisema ukweli wanalalamika.
 
Kauli ya John Kerry baada ya Kenyatta kutangazwa mshindi ni hii

"On behalf of the United States of America, I want to congratulate the people of Kenya for voting peacefully on March 4 and all those elected to office. Across the country, Kenyans turned out by the millions to exercise their most fundamental democratic right. I am inspired by the overwhelming desire of Kenyans to peacefully make their voices heard, and I applaud the patience they have shown as votes were tallied.Foremost in our minds is a desire to see the will of the Kenyan people expressed freely and fairly. We strongly urge all parties and their supporters to peacefully address any disputes with today's announcement by the Independent Electoral and Boundaries Commission through the Kenyan legal system, rather than on the streets. These elections are an historic opportunity for the people of Kenya to come together to build a better future. Since its independence in 1963, Kenya has been one of America's strongest and most enduring partners in Africa. We stand with you at this historic moment and will continue to be a strong friend and ally of the Kenyan people."
 
Jamani mbona yuko sahihi. Kule kaskazini mashariki Garissa kuna waandishi wa habari walitekwa. Mombasa na Lamu inabidi waingie kuripoti kimahesabu. Akisema ukweli wanalalamika.

Ukisoma comments za wakenya kwenye hiyo link kilichowaudhi ni kufananisha na Syria kwa sababu Syria serikali ndio problem na ndiyo inayofanya waandishi wapate shida lakini Kenya serikali imekuwa very supportive.

Hapa nadhani Obama genes zake za upande wa baba ndio zilizomuongoza.
 
Mimi nafikiri Wakenya wana over react kwa kuchagizwa na kilichotokea kabla ya hii statement, kwa maana kuwa, serikali za nchi za Magharibi hazikupenda Rais Uhuru achaguliwe, lakini ukiangalia pia mazingira aliyoisemea, utagundua kuwa ilikuwa ni mchanganyiko wa utani na vichekesho kama inavyotokea kwenye mikusanyiko ya press corps za USA
Paragraph yenyewe ni hii,
 
Inaweza kuwa tricks za kuinfluence kesi ya Raila ya uchaguzi. Sasa naanza kuhisi hii kesi kama ikifunguliwa inaweza kuwa na uzito mkubwa kuliko nilivyodhani awali!!!
ZeMarcopolo,
Umefatilia ule uzi wa Magwiji wapiganaji Wanasheria watakao iwakilisha CORD pale Supreme Court? ni Balaaaa tupu ndugu. Pia ile Barua ya Mungiki aliyoitoa CJ Dr Willy Mutunga Iliwachefua sana Uhruto..Kiasi kwamba inasemekana Wasingemwongeza Second Term. Sasa basi,nina wasiwasi Kunawezekana Uraisi ukawa wa Wiki mbili thereafter ukaota mbawa. Dr Willy Mutunga si Mkikuyu, so no guaranteed favour!
Yetu macho,
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…