- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa na baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook likidai kuwa aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama, amekamatwa baada ya Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump, kutoa amri hiyo kufuatia kile kinachoendelea Mashariki ya Kati.
Katika chapisho hilo linalosambaa, maneno yafuatayo yameonekana kuandikwa:“Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka Ikulu ya Marekani, wakati Trump anaandika ujumbe huo tayari Obama alikuwa ameshakamatwa.
Inaelezwa kuwa baada ya Donald Trump kufanya ziara nchini China, alirejea Marekani akiwa tofauti kabisa. Msemaji mkuu wa Trump amesema kuwa rais huyo alikwenda China kujua msimamo wa taifa hilo kuhusu usalama wa dunia na mustakabali wa amani duniani.
Uhalisia
Hata hivyo, kupitia ufuatiliaji uliofanywa kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya taarifa na nyenzo za utafutaji, hakuna sehemu yoyote iliyothibitisha kuwa Barack Obama amekamatwa au anahusishwa na makosa ya uhaini nchini Marekani.
Hakuna taarifa rasmi kutoka FBI, Idara ya Sheria ya Marekani (DOJ), wala mahakama yoyote inayothibitisha kukamatwa kwa Barack Obama.
Hatua hiyo imekuja baada ya kusambaa kwa chapisho lililomuonyesha Rais wa marekani Donald Trump akitoa tuhuma kali dhidi ya Barack Obama kupitia mtandao wake wa Truth Social.
Kwa mujibu wa taarifa hizo kutoka mtandao wa social truth ulinukuliwa kuwa;
“Rais Donald Trump aliendelea kumshambulia aliyekuwa Rais Barack Obama kupitia mfululizo wa machapisho kwenye Truth Social wiki hii, akimshutumu kwa uhaini na kutaka afikishwe mahakamani kwa madai ya makosa dhidi yake.
Katika mfululizo wa machapisho 55 yaliyowekwa kati ya saa 4:14 usiku wa Jumatatu Mei 11 hadi saa 7:12 usiku wa kuamkia Jumanne Mei 12, Trump alisambaza ujumbe uliotaka Obama akamatwe na kufikishwa mahakamani.
Baadhi ya machapisho hayo yalitoka kwenye akaunti kama @catturd2, huku mengine yakimtaja Obama kama ‘nguvu ya kishetani zaidi katika siasa za Marekani kwa miongo kadhaa.’
Machapisho hayo pia yalitoa madai yasiyo na uthibitisho yakidai Obama na washirika wake waliiba uchaguzi wa mwaka 2020 kutoka kwa Trump na kupanga njama za kuathiri uchaguzi wa mwaka 2016 dhidi yake.
Katika moja ya machapisho hayo, Trump alisambaza ujumbe uliosomeka:
''Wakamateni wote. Wafungulieni mashtaka wote. Wafungeni wote mara moja kwa uhaini, usaliti na njama za kuipindua serikali ya Marekani. Lakini wa kwanza awe Barack Obama.''
Hata hivyo, hadi sasa hakuna ushahidi rasmi unaothibitisha kuwa Barack Obama amekamatwa.